Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nidhamu yatajwa sababu Rashford kutemwa mechi tatu

Muktasari:

  • Hali imekuwa hivyo tena mwaka huu chini ya kocha mpya Ruben Amorim ambaye amemuacha staa huyo katika mechi tatu kabla ya mechi ya Wolves jana.

MANCHESTER, ENGLAND: IMEPITA miaka miwili tangu Marcus Rashford aachwe katika kikosi cha Manchester United kilichocheza dhidi ya Wolves chini ya kocha Erik ten Hag baada ya  kuchelewa kwenye mkutano wa timu.

Hali imekuwa hivyo tena mwaka huu chini ya kocha mpya Ruben Amorim ambaye amemuacha staa huyo katika mechi tatu kabla ya mechi ya Wolves jana.

Moja kati ya sababu zinazotajwa ni kwamba kocha huyo haridhishwi na kiwango cha Rashford mazoezini hali inayosababisha amuondoe, pia nidhamu yake ni mbovu.

Katika mahojiano yake mapema wiki hii, Amorim ameelezea kuwa Rashford anataka kucheza tena, lakini amekataa kusema atamrudisha lini uwanjani baada ya kumwacha katika mechi kadhaa zilizopita.

Hivi karibuni, Rashford mwenyewe alithibitisha kwamba yupo tayari kwa changamoto mpya na angependa kuachana na mashetani hao wekundu.

Amorim ambaye anapambana kuirudisha Man United katika mastari ikiwa imeshuka katika nafasi 10 za juu kwa mara ya kwanza tangu mwaka  1989, amesema kila mmoja ndani ya timu anafahamu nini Rashford anahitajika kufanya kwa ajili ya kurejea na tayari ameshaonyesha hali ya kupambana ili kurudi katika kikosi.

"Anataka kucheza. Anajitahidi. Nitamrudisha katika wakati ambao nitahisi kuwa ni  sahihi, kwa sasa naendelea kufikiria nini kinachofaa kwa timu."

Kocha huyu aliulizwa ikiwa suala la Rashford limeathiri utendaji wa timu  alisema hapana wote wanajua nini anahitaji.

" Kila mtu Carrington anajua ni nini ninachozungumza na nini nataka kutoka kwa Marcus na kila mchezaji mwingine. Nahitaji awe bora kutokana na kipaji chake, hivyo ndivyo ilivyo hata kwa wachezaji wengine ambao wapo hapa kwa sasa."