Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

NI VITA: Timu za England zamtolea udenda Pep Guardiola

kocha waklabu ya Batern Munich ya Ujerumani, Pep Guardiola

Muktasari:

Mkataba wa kocha huyo Allianz Arena unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu ujao, lakini ripoti kutoka kwao Hispania zinadai kwamba Guardiola atapata dili la kufundisha timu ya taifa ya Qatar katika michuano ya Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.

KIZURI chajiuza, kibaya chajitembeza. Hatima ya mkataba wa Kocha wa Bayern Munich, Pep Guardiola unaelekea kuzua zogo katika soka la England baada ya kocha huyo kuhusishwa kutua katika moja kati ya timu kubwa England.

Mkataba wa kocha huyo Allianz Arena unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu ujao, lakini ripoti kutoka kwao Hispania zinadai kwamba Guardiola atapata dili la kufundisha timu ya taifa ya Qatar katika michuano ya Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.

Hata hivyo, katika pengo la miaka sita kati ya mwaka 2016 na mwaka 2022, kocha anaweza kutumia muda huo kufundisha soka England kabla ya kwenda Qatar kufundisha timu hiyo ya taifa. Wakati mkataba wake wa sasa ukimalizika mwaka 2016, huo ndiyo mwaka ambao kocha Manuel Pellegrini wa Man City atakuwa anamaliza mkataba wake Etihad.

Guardiola pia anaweza kwenda Arsenal, Manchester United au Chelsea. Katika mwaka 2017, makocha Arsene Wenger, Louis van Gaal na Jose Mourinho watakuwa wanamaliza mikataba katika klabu zao.

Wakati Arsenal ikicheza soka kwa staili ambayo Guardiola anaitaka, Wenger anatarajiwa kustaafu kufundisha soka mwishoni mwa mkataba huu na Guardiola anaonekana kama mtu mwafaka zaidi kuchukua nafasi hiyo Emirates. Tajiri wa Chelsea, Roman Abramovich anajulikana kwa kuvutiwa na aina ya soka ambalo Guardiola anafundisha na mara kadhaa amewahi kumtaka kocha huyo bila ya mafanikio. Wakati wakala wa kocha Mourinho, Jorge Mendes akidai kwamba Mourinho anaweza kubaki Chelsea kwa miaka 10 ijayo, Abramovich hawezi kupoteza nafasi ya kumchukua Guardiola kama ikijitokeza.

Kabla ya kujiunga na Bayern, Guardiola aliwahi kumweleza mwandishi wa kitabu chake cha Herr Pep, Marti Perarnau, kuhusu uwezekano wa kufundisha soka England baada ya kumaliza muda wake Bayern. Katika kitabu hicho, Guardiola alidokeza kwa kusema; “Kabla ya kwenda England, nitaanzia Bayern na mwishowe itakuwa timu ya taifa.”