Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

NGUMI JIWE ULAYA! Arsenal vs PSV, Liverpool vs PSG

CL Pict

Muktasari:

  • Arsenal imepangwa kukipiga na PSV kwenye hatua hiyo, ambayo ukipigwa tu unatupwa nje - lakini kama Mikel Arteta na jeshi lake atafanikiwa kupenya, basi kwenye robo fainali atakabiliwa na mechi ya mshindi baina ya Real Madrid na Atletico Madrid. Mambo ni moto.

NYON, USWISI: ARSENAL, Liverpool na Aston Villa zimeshafahamu wapinzani gani watakutana nao kwenye raundi ya 16 bora ya mtoano kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya upangaji wa droo iliyofanyika Ijumaa.

Arsenal imepangwa kukipiga na PSV kwenye hatua hiyo, ambayo ukipigwa tu unatupwa nje - lakini kama Mikel Arteta na jeshi lake atafanikiwa kupenya, basi kwenye robo fainali atakabiliwa na mechi ya mshindi baina ya Real Madrid na Atletico Madrid. Mambo ni moto.

Aston Villa itakipiga na Club Brugge na Liverpool imepelekwa Ufaransa kuwakabili Paris Saint-Germain.

Kwenye droo hiyo, Liverpool imepewa kisiki cha maana. Baada ya Arne Slot kuvuka hatua ya makundi kwa kushinda mechi zake bila ya shida, kazi ipo kwenye mtoano wa 16 bora, kwa kupewa PSG. Na miamba hiyo ya Anfield kama itapenya kwenye kizingiti hicho, basi itakutana na mshindi kati ya Aston Villa na Club Brugge.

Arsenal ikipenya mbele ya PSV, itakwenda kukutana na ama Real Madrid au Atletico Madrid kwenye hatua inayofuata. Aston Villa iliyoonyesha balaa la kuichapa Bayern Munich, kutoka sare na Juventus, imepangwa na Club Brugge, ambayo inawafahamu vyema baada ya kukutana huko nyuma.

Mabingwa watetezi, Real Madrid wamepewa Madrid derby kwa kuwakabili Atletico Madrid, wakati hatua hiyo ya 16 bora itashuhudia mechi nyingine ya timu za ligi moja kumenyana zenyewe, ambapo miamba miwili ya Ujerumani, Bayer Leverkusen na Bayern Munich itamenyana wenyewe, huku Borussia Dortmund ikiwa na kibarua mbele ya Lille, wakati Feyenoord itakipiga na Inter Milan.

Barcelona itacheza na Benfica katika mechi nyingi matata kabisa, huku fainali ya mwaka huu za Ligi ya Mabingwa Ulaya itachezwa Jumamosi ya Mei 31 huko Munich, Ujerumani. Kwenye hatua hiyo ya 16 bora, mechi zitapigwa kati ya Machi 4/5 na zile za marudiano zitafanyika Machi 11/12.


RATIBA YENYEWE ILIVYO UEFA

Club Brugge vs Aston Villa

Borussia Dortmund vs Lille

Real Madrid vs Atletico Madrid

Bayern Munich vs Bayer Leverkusen

PSV Eindhoven vs Arsenal

Feyenoord vs Inter Milan

PSG vs Liverpool

Benfica vs Barcelona

ROBO FAINALI:

PSV/Arsenal vs Real Madrid/Atletico

PSG/Liverpool vs Brugge/Villa

Benfica/Barcelona vs Borussia Dortmund/Lille

Bayern/Leverkusen vs Feyenoord/Inter