Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ngoma imezidi viringe! Uholanzi yaichakaza Sweden mabao 5-1

Muktasari:

  • Ushindi huo umeiweka Uholanzi kileleni mwa Kundi F ikifikisha pointi nne baada ya kuanza na sare ya mabao 2-2 dhidi ya Japan.

HOUSTON, MAREKANI: TIMU ya Taifa ya Uholanzi, imeonesha ubora mkubwa katika Fainali za Kombe la Dunia 2026 baada ya kuitandika Sweden mabao 5-1, mchezo wa Kundi F uliochezwa leo Juni 20, 2026 kwenye Uwanja wa NRG uliopo Houston, Marekani.

Ushindi huo umeiweka Uholanzi kileleni mwa Kundi F ikifikisha pointi nne baada ya kuanza na sare ya mabao 2-2 dhidi ya Japan.

Kwa upande wa Sweden, iliingia kwenye mchezo huo ikiwa imetoka kupata ushindi wa aina hiyo dhidi ya Tunisia na kufanya kama vile nayo imeonjeshwa ladha ya kipigo kikali.

Mshambuliaji anayekipiga Sunderland, Brian Brobbey ndiye aliyeanza kufungua akaunti ya mabao kwa Uholanzi baada ya kufunga mabao mawili ya mapema dakika ya 5 na 17, akiiweka timu hiyo kwenye nafasi nzuri tangu mwanzoni mwa mchezo.

Uholanzi iliendelea kujipigia Sweden kipindi cha pili baada ya nyota wa Liverpool, Cody Gakpo, kufunga mabao mawili dakika ya 47 na 54 na kuiweka mbele timu hiyo kwa matokeo ya 4-0.

Wakati Sweden ikiendelea kupambana ili angalau kupunguza gepu la mabao, dakika ya 89 winga wa West Ham, Crysencio Summerville akafunga bao la tano.

Kabla ya hapo, Sweden ilipata bao lililofungwa na winga wa Newcastle, Anthony Elanga dakika ya 59, ambaye aliingia na kujaribu kuipa uhai timu hiyo, lakini juhudi zake hazikutosha kuzuia kasi ya mashambulizi ya Uholanzi. Elanga aliingia dakika ya 55 kuchukua nafasi ya Alexander Bernhardsson.

Katika mechi hiyo Uholanzi imeonekana kutawala maeneo mengi ya uwanja ikiongozwa na kiungo Frenkie de Jong, aliyerejea kikosini baada ya kuwa na changamoto ya kiafya kabla ya mchezo, huku mabeki wakiongozwa na nahodha Virgil van Dijk wakidhibiti vyema mashambulizi ya Sweden yaliyoongozwa na Alexander Isak na Viktor Gyokeres.

Mbali na mabao matano, Uholanzi imeonesha soka la kasi kupitia pembeni kwa msaada wa Denzel Dumfries, ambaye ametoa pasi mbili za mabao katika mchezo huo, huku Sweden ikishindwa kuhimili presha kubwa kutoka kwa vijana wa kocha Ronald Koeman.

Kabla ya mchezo huu, Sweden ilikuwa kinara wa kundi kutokana na ushindi mkubwa dhidi ya Tunisia, lakini matokeo ya leo yanaifanya Uholanzi kuwa karibu zaidi na hatua ya mtoano ikifikisha pointi nne kwenye mechi mbili.