Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Neymar Jr atinga kambini kwa ‘chopa’

NEYMAR Pict

Muktasari:

  • Brazil imeweka kambi katika kituo cha Columbia Park Training Facility kilichopo Morris Township, New Jersey, ambacho pia ni maskani ya mazoezi ya timu ya New York Red Bulls inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani (MLS). 

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil, Neymar Jr, amewasili kambini kwa mtindo wa kipekee kwa kutumia usafiri wa helikopta ‘Chopa’ nchini Marekani, tayari kwa maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia 2026. 

Brazil imeweka kambi katika kituo cha Columbia Park Training Facility kilichopo Morris Township, New Jersey, ambacho pia ni maskani ya mazoezi ya timu ya New York Red Bulls inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani (MLS). 

Kuwasili kwa mshambuliaji huyo kumeleta hamasa kubwa kufuatia mapokezi mazuri aliyopewa na kocha wa timu hiyo, Carlo Ancelotti, pamoja na wachezaji wenzake ambao tayari walishaanza mazoezi tangu mwanzoni mwa wiki hii.

NEY 01

Hata hivyo, mashabiki wa Brazil wataingia wasiwasi kidogo kwani staa huyo atalazimika kuanza na mazoezi mepesi pekee kutokana na jeraha dogo la misuli ya paja lililomlazimu kufanyiwa vipimo zaidi vya kitabibu. 

Jeraha hili linaweza kumfanya Neymar kukosa mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa Kombe la Dunia ambapo Brazil itamenyana na Morocco. 

NEY 02

Brazil imepangwa Kundi C ambalo linajumuisha pia mataifa ya Haiti na Scotland, hivyo benchi la ufundi litahitaji kufanya maamuzi ya tahadhari ili kulinda afya ya mchezaji huyo muhimu kwa mechi zinazofuata