Newcastle United yapata baba mzazi

Newcastle United yapata baba mzazi

NEWCASTLE, ENGLAND. RASMI Newcastle United imeuzwa kwa Pauni 300 milioni kwenda kwa matajiri wa mafuta kutoka nchini Saudi Arabia baada ya kumilikiwa kwa muda mrefu na mfanya biashara Mike Ashley.
Ashley alimiki timu hiyo kwa miaka 14 na katika siku za hivi karibuni kulikuwa na maandamano ya mashabiki wakihitaji aondoke kwani timu haikupata mafaniko yoyote makubwa katika kipindi chake.
Baada ya kuuzwa mmiliki halali wa timu hiyo kuanzia sasa ni Mohammad bin Salman ambaye ndio mwenyekiti wa  Saudi Arabia Public Investment Fund ambayo imechukua hisa za asilimia 80 huku 20 zilizosalia zikienda kwa bilionea Reuben brother na  Amanda Staveley ambao kila mmoja anamiliki asilimia 10.
Taarifa zinadai huo ndio utakuwa mwisho wa kocha wa timu hiyo Steve Bruce kwa sababu mmiliki mpya atahitaji kufanya maboresho ya timu nzima.
Kununuliwa huko kwa Newcastle kumeifanya itambulike kama timu inayomilikiwa na mmoja kati ya matajiri wakubwa Duniani ikiungana na  Manchester City na  Paris Saint-Germain.