Newcastle kufanya ujanja Isak abaki
Muktasari:
- Fowadi huyo mwenye umri wa miaka 25 alifunga bao lake la 16 na 17 kwenye Ligi Kuu England baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Southampton wikiendi iliyopita. Na kutokana na hilo, Newcastle inataka kufanya straika huyo kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi kwenye timu yao.
NEWCASTLE, ENGLAND: NEWCASTLE United inajiandaa kumpa dili tamu straika Alexander Isak ili kukata ngebe za timu zinazohitaji saini yake ikiwamo Arsenal, imeelezwa.
Fowadi huyo mwenye umri wa miaka 25 alifunga bao lake la 16 na 17 kwenye Ligi Kuu England baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Southampton wikiendi iliyopita. Na kutokana na hilo, Newcastle inataka kufanya straika huyo kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi kwenye timu yao.
Isak bado ana mkataba wa miaka minane na nusu katika kikosi hicho na sasa kinachotaka kufanyika ni kuboresha mapato ya mchezaji huyo.
Baada ya kuanza kuzungumzia hilo mwaka jana na sasa kinachoelezwa ni kwamba mazungumzo yataanza upya mwisho wa msimu.
Kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya ni kitu kitakachofanya mazungumzo hayo kwa sababu zitamfanya Isak kufuta kabisa mpango wa kuondoka kwenye timu hiyo.
Kinachoelezwa ni kwamba Isak anafurahia maisha Newcastle na wachezaji wenzake wala hawafikirii kama anataka kwenfa kwingineko.
Mabosi wa Newcastle United waliripotiwa kutaka Pauni 150 milioni kwenye dili la kumuuza Isak kwenye dirisha la uhamisho wa majira ya kiangazi mwaka jana.
Arsenal imekuwa ikihusishwa na straika huyo wa kimataifa wa Sweden. Lakini, ripoti zinafichua kwamba Arsenal haitaweza kumudu za mchezaji huyo.
Isak atakuwa na nafasi ya kuwaonyesha shoo Arsenal wakati watakaporudiana kwenye nusu fainali ya Kombe la Ligi, Februari 5.
Newcastle ilishinda 2-0 katika mchezo wa kwanza na kuweka matumaini ya kuvuka ili kwenda kutimiza ndoto za kubeba taji lao la kwanza tangu 1955.