Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Neville atoa utabiri mpya Man United

Muktasari:

  • Mashetani Wekundu walipata ushindi wa sita katika michezo saba chini ya Carrick, Jumapili walitoka nyuma kwa bao 1-0 na kuifunga Crystal Palace 2-1.

MANCHESTER, ENGLAND: GARY Neville amekiri kuwa haamini sasa anaitabiria Manchester United kumaliza katika nafasi ya tatu, akizingatia walipokuwa kabla ya Michael Carrick kuchukua mikoba kutoka kwa Ruben Amorim.

Mashetani Wekundu walipata ushindi wa sita katika michezo saba chini ya Carrick, Jumapili walitoka nyuma kwa bao 1-0 na kuifunga Crystal Palace 2-1.

Mfululizo huo mzuri umeifanya timu hiyo kuwakaribia vigogo wawili wa juu, Arsenal na Manchester City, huku sasa wakiwa katika nafasi nzuri ya kurejea kwenye mikikimikiki ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Man United imezipita Chelsea, Liverpool na Aston Villa baada ya kukusanya pointi 19 kati ya 21 zinazowezekana. Sasa Neville, ambaye mara nyingi huibashiria timu yake ya zamani kumaliza katika nne bora anaamini kweli watafanikisha hilo.

Akizungumza kwenye The Gary Neville Podcast, alisema: “Nadhani United itamaliza nafasi ya tatu bila shaka. Siwezi kuamini nasema hivi ukizingatia walipokuwa wiki sita zilizopita. Lakini, hawana usumbufu wa mashindano mengine, kuna kitu kizuri kinaendelea, wana kasi na morali.

“Nadhani Liverpool watamaliza wa nne na Chelsea wa tano. Natumaini Aston Villa itamaliza katika tano bora, kweli natumaini. Nimesema kabla kuwa kocha wao ni mtu mwenye uzoefu na busara. Wakipata baadhi ya wachezaji wao walioumia hasa viungo hilo limewagharimu.”

Timu zinazowania kufuzu taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya bado zinatarajiwa kukutana katika hatua za mwisho za msimu. Ndani ya wiki mbili zijazo, Man United itaikaribisha Aston Villa, kisha itasafiri kwenda Stamford Bridge kuikabili Chelsea na pia watawakaribisha Liverpool. Kulingana na matokeo ya michezo hiyo, picha ya tano bora inaweza kubadilika tena. Man United ndio timu pekee kati ya hizo isiyoshiriki mashindano ya Ulaya msimu huu, jambo linalowapa muda zaidi wa maandalizi na kupunguza uchovu wa kikosi.