Nani Bruno? Wala hawasikii
Muktasari:
- Lakini, Fernandes, 31, alisema hasumbuki na hayo maneno ya watu na kusema kwamba hawezi kubadili namna alivyo kwa kuwasikiliza watu. “Watu wamekuwa wakisema sana kuhusu mimi, siwezi kubadilika,” alisema Fernandes na kuongeza.
MANCHESTER, ENGLAND: KIUNGO fundi wa boli, Bruno Fernandes ataiongoza Manchester United, Jumapili hii kwenye kipute cha Manchester derby na kusema tena kwa msisitizo, hawezi kubadili staili yake ya uchezaji licha ya kukosolewa sana.
Nahodha huyo wa Man United amekuwa akikosolewa sana kutokana na kucheza kwa huruma sana uwanjani, wengi wakidai kwamba hana ule moyo unaotakiwa wa kuvaa kitambaa cha miamba hiyo ya Old Trafford.
Lakini, Fernandes, 31, alisema hasumbuki na hayo maneno ya watu na kusema kwamba hawezi kubadili namna alivyo kwa kuwasikiliza watu. “Watu wamekuwa wakisema sana kuhusu mimi, siwezi kubadilika,” alisema Fernandes na kuongeza.
“Ndivyo walivyoamua kuhukumu kwa kila wanachokiona, kile wanachotaka kukiona uwanjani na wengine wamekuwa wakiona tu kwenye televisheni. Sote tuna maoni, tena maoni tofauti na ndio maana ya maisha.”
Staa huyo wa zamani wa Sporting CP alisema familia yake na marafiki wanamwona mtu tofauti kabisa na kwamba yeye kitu ambacho kipaumbele chake kwa sasa ni kucheza soka tena la kiwango kinavyokubalika.
“Kila kitu, kile unachokiona uwanjani, hivyo ndivyo Bruno alivyo. Kwa namna ninavyojitolea kwa kila kitu, nipo hivyo hata nikiwa nje ya uwanja.”