Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwenendo wa Spurs wamwibua Daniel Levy

LEVY Pict

Muktasari:

  • Levy amesema hakuwahi kutarajia Spurs kuwa katika hali ya kupambana na hatari ya kushuka daraja kutokana na misingi iliyokuwepo kwa wakati huo.

LONDON, ENGLAND: ALIYEKUWA mwenyekiti wa Tottenham Hotspurs, Daniel Levy, amezungumza hadharani kwa mara ya kwanza kuhusu klabu hiyo tangu alipoondolewa madarakani Septemba mwaka jana baada ya kudumu kwa zaidi ya miaka 23 madarakani.

Levy amesema hakuwahi kutarajia Spurs kuwa katika hali ya kupambana na hatari ya kushuka daraja kutokana na misingi iliyokuwepo kwa wakati huo.

"Ninahisi maumivu lakini nina matumaini tutapita kipindi hiki,” amesema Levy mwenye umri wa miaka 64 alipookuwa akifanya mahojiano na Sky Sports baada ya kupokea tuzo yake ya CBE katika hafla iliyofanyika Windsor Castle.

LEV 01

“Imekuwa ngumu sana lakini Spurs ipo kwenye damu yangu na nina matumaini mwishowe tutakuwa salama. Sikuwahi kuwaza kitu kama hiki. Kwa hakika nimevunjika moyo sana lakini tuangalie mbele na kuwa na matumaini mwaka ujao tutakuwa bado katika Ligi Kuu. Mimi siku zote nina matumaini na ninaomba kila siku."

Kwa sasa Spurs ina alama mbili zaidi ya timu zilizo kwenye mstari wa kushuka daraja ukiwa na pointi 38, idadi sawa kabisa ya pointi ilizomaliza nazo msimu uliopita katika EPL.

Msimu uliopita pointi hizo zilitosha kuwabakisha Ligi Kuu, lakini safari  mambo yanaonekana kuwa magumu huku zikiwa zimebaki mechi mbili tu kabla ya ligi kuisha.

Kwa sasa Spurs ina vita kali na West Ham United ambayo ndio inagombania naye na mmoja wao lazima ashuke ili mwingine abaki.

LEV 02

Levy, ambaye alisimamia ujenzi wa uwanja wa kisasa wa Tottenham Hotspur Stadium, aliondolewa Spurs kufuatia mabadiliko ya uongozi yaliyoongozwa na familia ya Lewis inayomiliki klabu hiyo.

Peter Charrington alichukua nafasi yake kama mwenyekiti asiyehusika moja kwa moja na shughuli za kila siku, huku majukumu ya kuendesha klabu yakikabidhiwa kwa Mtendaji Mkuu Vinai Venkatesham.

Levy alikuwa amemteua Venkatesham Aprili 2025 na katika mahojiano yao ya pamoja msimu uliopita walizungumza kuhusu ndoto ya kushinda mataji makiubwa.

Hata hivyo, chini ya mwaka mmoja baadaye, Tottenham sasa wanapambana kuepuka kushuka daraja kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1977.