Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwandishi: Bado natetemeka Messi kushangilia na mimi

Muktasari:

  • Tukio hilo lilijiri jana baada ya Messi kuifungia Argentina bao la pili kwenye mchezo dhidi ya Austria, ambapo mabingwa hao watetezi wa Kombe la Dunia wakipata ushindi wa pili mfululizo wa mabao 2-0.

Mtangazaji wa kituo cha Tyc Sports kutoka Argentina, Juaquin Bruno, amesema mpaka sasa bado anashangaa hatua ya mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi kushangilia naye bao, hali ambayo akikumbuka anajikuta akitetemeka.

Tukio hilo lilijiri jana baada ya Messi kuifungia Argentina bao la pili kwenye mchezo dhidi ya Austria, ambapo mabingwa hao watetezi wa Kombe la Dunia wakipata ushindi wa pili mfululizo wa mabao 2-0.

Bruno amesema hakutarajia tukio hilo ambapo kila akikumbuka namna Messi alivyomfuata eneo ambalo alikuwa amekaa, anajikuta anafurahia furaha ya mshambuliaji huyo.

"Mpaka sasa bado siamini kabisa. Kila nikikumbuka natetemeka namna Messi alivyokuja kushangilia nami lile bao lake la pili tena pale nilipokuwa nimekaa," amesema Bruno.

"Tukio lile lilikuwa la haraka sana, aliniona nikishangilia kwa furaha, tukakutana machoni wote tukiwa na furaha, kisha akanifuata na kunipa mkono, ilikuwa spesho sana, nikikumbuka najikuta mwenye furaha usoni na moyoni."

Mesii kwenye mchezo huo alifunga mabao mawili yaliyomfanya kuwa kinara wa ufungaji kwenye fainali za msimu huu akifikisha mabao matano, lakini pia akiweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa jumla akifunga mabao 18.