Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwamba Bruno Fernandes ajiunga na klabu ya wakali wa asisti

Muktasari:

  • Mashetani Wekundu walipanda hadi nafasi ya sita juzi baada ya kushinda mabao 4-1 ugenini dhidi ya Wolves, huku nahodha Bruno akiibuka nyota katika Uwanja wa Molineux.

WOLVEHAMPTON,  ENGLAND: STAA wa Manchester United, Bruno Fernandes amejiunga na klabu ya wakali wa asisti baada ya kufanikiwa kutoa asisti ugenini huku Manchester United ikiingia sita bora katika Ligi Kuu England, baada ya miezi zaidi ya 30.

Mashetani Wekundu walipanda hadi nafasi ya sita juzi baada ya kushinda mabao 4-1 ugenini dhidi ya Wolves, huku nahodha Bruno akiibuka nyota katika Uwanja wa Molineux.

Kikosi hicho cha kocha Ruben Amorim kilitangulia kwa bao lililofungwa na nahodha wao huyo katika kipindi cha kwanza baada ya kubutua mpira ukamwacha kipa wa Wolves, Sam Johnstone akiduwaa na kujaa wavuni.

Hata hivyo, muda mfupi baaday Jean-Ricner Bellegarde alisawazisha, Bryan Mbuemo aliirejeshea Man United uongozi na kisha Fernandes akatoa asisti ya bao kwa Mason Mount kufunga la tatu, na kisha akafunga bao lake la pili kupitia mkwaju wa penalti dakika kumi kabla ya mchezo kumalizika.

Bruno alifunga mabao mawili, lakini kupitia asisti yake ya bao ndipo alipojiunga rasmi na klabu ya wachezaji watano pekee waliofanya hivyo mara tano mfululizo ugenini katika mashindano hayo tangu yalipoanzishwa 1992-93.

Mfululizo wake ulianza Oktoba, mwaka huu, alipoasisti bao la Harry Maguire dhidi ya Liverpool huko Anfield kisha akawapa Casemiro dhidi ya Nottingham Forest na Matthijs de Ligt walipokutana na Tottenham Hotspur.

Pasi mbili zaidi alizitoa katika ushindi dhidi ya Crystal Palace huko Selhurst Park, Novemba 30, kabla ya juzi Jumatatu kutoa ya tano. Mfululizo huo umemfanya aingie kwenye kundi la wachezaji wachache waliofanikiwa kufanya hivyo.

Mohamed Salah wa Liverpool anayetikisa vichwa vya habari kutokana na kauli yake ya hivi karibuni kulalamika kusugulishwa benchi ni mmoja wa mastaa wa Ligi Kuu England waliowahi kutoa asisti mara tano mfululizo 2023, huku Gerard Deulofeu, staa wa zamani wa Everton 2015 ilhali gwiji wa Arsenal, Cesc Fàbregas, alifanya hivyo akiwa Chelsea msimu wa 2014/15 wakati staa wa zamani wa Leicester City, Muzzy Izzet, ndiye aliyekuwa wa kwanza kufanya hivyo 2003.


BRUNO WAMOTO

Zaidi ya hilo, takwimu za Bruno zimeanza kumfanya afanane na majina makubwa Ulaya akiwa na asisti sita msimu huu, huku juu yake kukiwa na mastaa wawili pekee ambao ni Michael Olise wa Bayern Munich (nane) na Lamine Yamal (Barcelona, saba).

Kwa kufunga na kutoa asisti dhidi ya Wolves, Fernandes ameifikisha mechi 16 ambazo amefunga na kutoa pasi ya bao ndani ya mchezo mmoja. Ni Salah (27) na Kevin De Bruyne (17) tu ambao wamefanya hivyo mara nyingi zaidi tangu Bruno aanze kucheza England.

Hii pia ilikuwa mara ya nane kwake kuhusika moja kwa moja kwenye mabao matatu ndani ya mchezo mmoja wa ligi hiyo, na mara ya kwanza tangu Machi msimu uliopita dhidi ya Leicester city.

Winga wa Man United, Mason Mout akizungumzia asisti aliyopewa na Bruno, alisema: “Mara tu nilipomuona akiwa na mpira, ilikuwa ishara kwangu kukimbia nyuma ya safu ya ulinzi ya Wolves. Tunajua ubora wake na mara tu akipata mpira ‘anaskani’ nafasi kisha anakutupia uhangaike na bao.

“Ni furaha kucheza naye unapocheza juu uwanjani... unajua tu ataangalia na kukuletea mpira mzuri juu ya mabeki.”