Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msako wamkata umeme unaendelea Old Trafford!

BALEBA Pict

Muktasari:

  • Ruben Amorim alitumia pesa nyingi dirisha lililopita la majira ya kiangazi kuboresha safu yao ya ushambuliaji, hivyo ilipungukiwa pesa kwenye kuboresha sehemu ya kiungo na inahitaji kiungo mkabaji. Machaguo ya Man United kwenye sehemu ya kiungo imekuwa ikizua maswali mengi kwa msimu huu na kocha Amorim amekuwa akiwatumia sana Casemiro na Bruno Fernandes katika eneo hilo.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United itaweka kipaumbele chake kwenye kuboresha sehemu ya kiungo wakati itakapoingia sokoni dirisha lijalo la usajili, huku masupastaa Carlos Baleba na Conor Gallagher wametajwa kuwa miongoni mwa sita inaowasaka.

Ruben Amorim alitumia pesa nyingi dirisha lililopita la majira ya kiangazi kuboresha safu yao ya ushambuliaji, hivyo ilipungukiwa pesa kwenye kuboresha sehemu ya kiungo na inahitaji kiungo mkabaji. Machaguo ya Man United kwenye sehemu ya kiungo imekuwa ikizua maswali mengi kwa msimu huu na kocha Amorim amekuwa akiwatumia sana Casemiro na Bruno Fernandes katika eneo hilo.

Lakini, mkataba wa Casemiro unakaribia ukingoni, Fernandes naye amekuwa akihusishwa sana na mpango wa kuondoka kwenye kikosi hicho cha Old Trafford, huku kiungo bwana mdogo Kobbie Mainoo bado hajaonyesha kile ambacho Amorim anakitaka.

BEL 01

Kiungo wa Brighton, Baleba alihusishwa na mpango wa kutua Man United kwa ada ya Pauni 100 milioni dirisha lililopita, lakini dili hilo lilishindwa kutimia. Kiwango chake kimeshuka kiasi msimu huu huko Amex, lakini Man United bado inahitaji saini yake na imemweka kwenye mipango ya wachezaji inaowasaka kwenye eneo hilo la kiungo.

Nahodha wa zamani wa Chelsea, Gallagher alihusishwa kutua kwa mkopo Man United, lakini Atletico Madrid ilichotaka ni kumuuza jumla, hivyo dili hilo lilikwama. Amecheza dakika chache msimu huu na hilo limemfanya afikirie kurudi England, lakini dili lake kutimia lina ugumu.

Viungo wengine wawili wa kizazi kipya cha England nao wapo kwenye rada ya Man United. Adam Wharton na Elliot Anderson wamekuwa kwenye kiwango bora na hilo linawafanya Man United kuwaweka kwenye mpango wa kunasa saini zao.

Kiungo Wharton ana mkataba huko Crystal Palace hadi 2029 na hajaonyesha dalili yoyote ya kutaka kuhama na kama ataondoka, basi saini yake itahitaji pesa ndefu sana. Hali hiyo pia ni sawa na Anderson kwenye kikosi cha Nottingham Forest, licha ya timu kusuasua. Newcastle imehusishwa na mpango wa kutaka kurudi kwa Anderson, ambaye ameanza kufikiria kuhamia kwenye klabu kubwa ili kwenda kupandisha ubora wa soka lake.

BEL 02

Mkali wa Chelsea, Andrey Santos naye yumo kwenye mipango ya Man United. Mbrazili huyo aliwahi kutajwa kuhusishwa kwenye dili la kutua Man United hasa katika kile kipindi ambacho kimemshuhudia Alejandro Garnacho akiondoka Old Trafford kwenda Stamford Bridge.

Santos alikuwa Strasbourg msimu uliopita na alikuwa akitaka kuondoka dirisha lililopita la majira ya kiangazi, lakini alitaka kuipa Chelsea nafasi ya kuonyesha kiwango chake kabla ya kufungasha virago na kwenda kutafuta malisho mapya.

Staa mwingine, ambaye jina lake si maarufu, ambaye anatajwa kwenye mpango huo wa Man United ni Angelo Stiller wa Stuttgart. Man United inamfuatilia kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani, ambaye pia ameweka wazi milango ya kutua Ligi Kuu England. Stiller kwenye mkataba wake kuna kipengele kinachotaja bei inayotosha kuvunjwa kwa dili hilo kuwa ni Pauni 35 milioni, lakini Stuttgart inaruhusu ya kulipa Pauni 1.5 milioni tu kukiondoa kipengele hicho kwenye mkataba wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24.