Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha: Man United imemvuruga Baleba

BALEBA Pict

Muktasari:

  • Baleba alihusishwa sana na mpango wa kutua huko Old Trafford katika dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi na alikuwa kwenye mipango ya kocha Ruben Amorim akacheze Namba 6 sambamba na Bruno Fernandes kwenye safu ya kiungo.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Brighton, Fabian Hurzeler amekiri kiungo wake Carlos Baleba ameathiriwa na kelele za kuhusu kukwama kwa dili lake la kwenda kujiunga na Manchester United.

Baleba alihusishwa sana na mpango wa kutua huko Old Trafford katika dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi na alikuwa kwenye mipango ya kocha Ruben Amorim akacheze Namba 6 sambamba na Bruno Fernandes kwenye safu ya kiungo.

Lakini, Man United iliweka kando mpango wa kumchukua staa huyo baada ya Brighton kumthaminisha kuwa na thamani ya Pauni 115 milioni.

Hurzeler alisema alikuwa na uhakika Baleba asingeuzwa, lakini hakufahamu kama jambo hilo lingekuwa na madhara makubwa kwa mchezaji huyo. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21 aliwekwa kwenye benchi wakati timu hiyo ilipochapwa 2-1 na Bournemouth kwenye mchezo wa Ligi Kuu England, Jumamosi iliyopita.

Kocha huyo Mjerumani alisema Baleba ameathirika kiakili kuhusu uvumi wa uhamisho wake kwenda Man United, akisema: “Si kitu kizuri kwa wachezaji vijana kukumbana nacho.”

“Nadhani hicho ni kitu cha kawaida kwa wachezaji vijana wanapozongwa na vyombo vya habari. Ni ngumu sana kwa wachezaji wa umri kama wake kukabiliana nayo. Hivyo, tunahitaji kumpa muda na sapoti kubwa ili arudi kwenye viwango vyake bora.”

Hurzeler alifichua hilo baada ya mechi ya Bournemouth, ambapo Baleba alitokea benchini na kucheza dakika 24 za mwisho.

Hiyo ilikuwa mara ya kwanza Baleba kutoanzishwa kwenye mchezo wa Ligi Kuu England msimu huu. Amecheza dakika 200 kwenye ligi msimu huu na amekuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Brighton tangu alipowasili mwaka 2023.

Amecheza mechi 82 katika timu hiyo, akifunga mabao manne na kuwa mmoja wa viungo bota waliofanikiwa Brighton akifuata nyayo za wakali Yves Bissouma, Moises Caicedo na Alexis Mac Allister, ambao wote wameuzwa na klabu hiyo.