Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mpishi amfungulia kesi Neymar

MPISHI Pict

Muktasari:

  • Mpishi huyo pia anadai kuwa alipata majeraha ya mwili alipokuwa akiandaa chakula katika moja ya makazi ya Neymar huko Rio de Janeiro, Brazil. Nyota huyo wa zamani wa Barcelona alirudi nchini Brazil baada ya kipindi kigumu nchini Saudi Arabia, na sasa anaishi katika eneo la Mangaratiba karibu na Rio de Janeiro.

RIO DE JANEIRO, BRAZIL: SUPASTAA, Neymar anakabiliwa na kesi ya kisheria kutoka kwa mpishi wake binafsi ambaye anadai fidia ya fedha baada ya kulazimishwa kufanya kazi hadi saa 16 kwa siku na wakati mwingine kupika chakula cha hadi watu 150.

Mpishi huyo pia anadai kuwa alipata majeraha ya mwili alipokuwa akiandaa chakula katika moja ya makazi ya Neymar huko Rio de Janeiro, Brazil. Nyota huyo wa zamani wa Barcelona alirudi nchini Brazil baada ya kipindi kigumu nchini Saudi Arabia, na sasa anaishi katika eneo la Mangaratiba karibu na Rio de Janeiro.

Inasemekana Neymar anamiliki majengo mawili ya kifahari na mpishi huyo alifanya kazi katika eneo linaloitwa Casa Hotel Portobello kuanzia Julai 2025 hadi Februari mwaka huu.

Mpishi huyo amefungua kesi katika Mahakama ya Kazi ya Mkoa wa Kwanza nchini Brazil, akidai kuwa alilazimika kufanya kazi hadi saa 16 kwa siku kwa ajili ya Neymar, jambo lililomlazimu kuandaa chakula kwa mchezaji huyo pamoja na hadi watu 150 ambao ni marafiki na washirika wake karibu kila siku.

Kwa mujibu wa mkataba wa awali, alitakiwa kufanya kazi kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 11 jioni kuanzia Jumatatu hadi Alhamisi na kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 10 jioni siku ya Ijumaa. Hata hivyo, mpishi huyo anadai mara nyingi alilazimika kufanya kazi hadi saa 5 usiku au hata saa 6 usiku, pamoja na kufanya kazi mwishoni mwa wiki. Pia anasema mara nyingi alifanya kazi bila kupata muda wake wa mapumziko wa chakula cha mchana ambao kisheria alipaswa kupewa.

Mpishi huyo anadai pia alipata majeraha ya mwili kutokana na kazi nzito, ikiwemo kubeba vipande vya nyama vyenye uzito wa takribani kilo 10 kila kimoja pamoja na kubeba na kushusha mifuko mizito. Inasemekana alipata matatizo ya mgongo na uvimbe kwenye nyonga.

Kutokana na hali hiyo, mpishi huyo wa zamani wa Neymar ambaye alikuwa akilipwa takribani Pauni 1,065 kwa mwezi (reais 7,500 za Brazil), anadai fidia ya Pauni 37,544 (reais 262,000 za Brazil). Kiasi hicho kinajumuisha malipo ya kuachishwa kazi, faini, malipo ya saa za ziada, malipo ya muda wa mapumziko ambao hakupata, fidia ya uharibifu alioupata pamoja na gharama za matibabu.