Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mourinho adai hatamsahau Anthony Taylor

MOURINHO Pict

Muktasari:

  • Katika fainali hiyo iliyochezwa mwaka 2023, Roma ilipoteza kwa mikwaju ya penalti dhidi ya Sevilla baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 120. Baada ya mchezo huo, Mourinho alionekana mwenye hasira kubwa na aliwashutumu waamuzi wa mechi hiyo wakiongozwa na Taylor.

MADRID, HISPANIA: KOCHA mpya wa Real Madrid, Jose Mourinho amesema bado hajasahau maumivu ya kupoteza fainali ya Europa League akiwa na Roma, akisisitiza kama angepewa nafasi ya kurudia mchezo mmoja katika maisha yake ya ukocha, angechagua fainali hiyo dhidi ya Sevilla, lakini bila mwamuzi Anthony Taylor.

Mourinho, ambaye amerejea Real Madrid kwa awamu ya pili ya ukocha wake, alitoa kauli hiyo katika mahojiano maalumu na podikasti ya Beast Mode On, akionyesha bado ana kinyongo na mwamuzi huyo wa England kutokana na maamuzi aliyodai yalichangia timu yake kupoteza taji hilo mwaka 2023.

Katika fainali hiyo iliyochezwa mwaka 2023, Roma ilipoteza kwa mikwaju ya penalti dhidi ya Sevilla baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 120. Baada ya mchezo huo, Mourinho alionekana mwenye hasira kubwa na aliwashutumu waamuzi wa mechi hiyo wakiongozwa na Taylor.

MOU 01

Alipoulizwa ni mchezo gani angependa urudiwe, Mourinho amesema: “Roma dhidi ya Sevilla katika fainali ya Europa League, lakini bila Anthony Taylor.”

Akiwa Roma, Mourinho aliandika historia kwa kuwa kocha wa kwanza kushinda mashindano yote matatu ya klabu Ulaya chini ya UEFA; Ligi ya Mabingwa Ulaya, Kombe la UEFA/Europa League na Europa Conference League.

Mreno huyo aliiongoza Roma kutwaa taji la kwanza la Europa Conference League mwaka 2022 baada ya kuifunga Feyenoord ya Uholanzi kwenye fainali. Ushindi huo ulihitimisha ukame wa miaka 11 wa Roma bila taji kubwa.

MOU 02

Mourinho amesema mafanikio hayo akiwa Roma ni miongoni mwa mafanikio makubwa zaidi katika maisha yake ya ukocha wa miaka 26.

“Nilifanya mambo mengi makubwa, lakini tuliposhinda Conference League, jiji lote la Roma lilichanganyikiwa kwa furaha. Tulifanya kitu ambacho hata washindi wa Ligi ya Mabingwa hawawezi kufanya katika baadhi ya miji mingine,” amesema Mourinho.

Kocha huyo pia alieleza mashabiki wa Roma wana mapenzi makubwa na klabu yao kuliko sehemu nyingi duniani na ndiyo sababu mafanikio hayo yana nafasi ya kipekee moyoni mwake.

MOU 03

Mbali na hilo, Mourinho alitaja Uwanja wa Anfield wa Liverpool kuwa uwanja mgumu zaidi kuwahi kuchezea akiwa kocha wa timu mbalimbali.

Mourinho sasa anarejea Santiago Bernabeu akiwa na jukumu la kuirejesha Real Madrid kwenye mafanikio makubwa, baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu. Katika kipindi chake cha kwanza kati ya mwaka 2010 na 2013, aliiongoza Madrid kutwaa mataji ya LaLiga na Copa del Rey.

Akiwa Madrid kwa mara nyingine, Mourinho anatarajiwa kufanya kazi na nyota wakubwa akiwemo Jude Bellingham, Kylian Mbappe na Vinicius Junior huku mashabiki wakitarajia kuona kama ataweza kurejesha enzi zake za mafanikio ndani ya klabu hiyo.