Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Morocco yajipigia Scotland, Saibari wa moto

Muktasari:

  • Dakika ya kwanza Morocco ikafanikiwa kuandika bao pekee lililoamua mchezo huo, mfungaji akiwa Saibari kwa shuti kali, akipokea pasi ndefu ya kiungo wake Brahimi Diaz.

Morocco imeendelea kuonyesha ubora wa soka baada ya kuichapa Scotland kwa bao 1-0 huku mshambuliaji wake Ismael Saibari akizidi kuonyesha ubora.

Dakika ya kwanza Morocco ikafanikiwa kuandika bao pekee lililoamua mchezo huo, mfungaji akiwa Saibari kwa shuti kali, akipokea pasi ndefu ya kiungo wake Brahimi Diaz.

Bao hilo limekuwa la pili kwa Saibari ambaye ndiye mchezaji bora wa Ligi ya Uholanzi, ambapo kwenye mchezo wa kwanza Morocco ikipata sare dhidi ya Brazil bao lake ndio lililowabeba Waarabu hao.

Morocco licha ya kutengeneza nafasi nyingi ikashindwa kuzitumi, ilifanikiwa kuibana Scotland iliyoshindwa kufanya mashambulizi makubwa kusawazisha bao hilo.

Morocco ambayo ikitawala kwa umiliki wa mpira kwa vipindi vyote, ukuta wao ulikuwa mzito ukiifanya Scotland kumaliza dakika 90 bila kupiga shuti lililolenga lango.

Licha ya dakika 10 za mwisho Scotland kupeleka presha kwa Morocco lakini mashambulizi yake yakazimwa kirahisi na ukuta wa Waarabu hao.

Ushindi huo unaifanya Morocco kuongoza kundi lao C ikifikisha pointi nne wakati Scotland ikiwa nafasi ya pili na pointi zake tatu,Brazil ambayo itashuka uwanjani saa chache baadaye ikiwa na moja huku Haiti ikiwa haina kitu.