Alimwa umeme kwa kufunika mdomo Kombe la Dunia
Muktasari:
- Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa kipindi cha kwanza cha mchezo wa Kundi D anaochezwa asubuhi ya leo, Jumamosi kati ya Paraguay dhudi ya Uturuki baada ya mshambuliaji wa Paraguay, Isidro Pitta, kuchezewa faulo na kuzua mvutano kati ya wachezaji wa timu hizo mbili.
CALIFORNIA, MAREKANI: NYOTA wa Paraguay, Miguel Almiron amejikuta akiweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kosa la kuongea akiwa amefunika mdomo katika mchezo wa Kombe la Dunia 2026.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa kipindi cha kwanza cha mchezo wa Kundi D anaochezwa asubuhi ya leo, Jumamosi kati ya Paraguay dhudi ya Uturuki baada ya mshambuliaji wa Paraguay, Isidro Pitta, kuchezewa faulo na kuzua mvutano kati ya wachezaji wa timu hizo mbili.
Nyota huyo alionyeshwa kadi hiyo kufuatia kufunika mdomo wakati akizungumza na beki wa Uturuki, Mert Müldür.
Mwamuzi kutoka El Salvador, Iván Barton, hakuliona tukio hilo mara moja lakini aliarifiwa na waamuzi wa VAR ambao walimwelekeza kuangalia upya tukio hilo kabla ya kutoa kadi nyekundu kwa Almiron.
Sheria hiyo mpya ilianza kutumika kabla ya Kombe la Dunia baada ya tukio lililomhusisha kiungo wa Benfica, Gianluca Prestianni, aliyedaiwa kufunika mdomo wake wakati akitoa maneno ya kibaguzi kwa nyota wa Real Madrid, Vinicius Junior, katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mapema mwaka huu.
Kwa mujibu wa bodi ya sheria za soka duniani, waandaaji wa mashindano wana mamlaka ya kumwadhibu kwa kadi nyekundu mchezaji yeyote anayefunika mdomo wake katika mazingira ya ugomvi au mzozo na mpinzani wake.
Awali, wachezaji na makocha walikuwa wakifunika midomo yao ili kuficha maelekezo ya kiufundi au mazungumzo yasinaswe na kamera za televisheni, lakini sasa kitendo hicho kinaweza kugharimu timu kutokana na kanuni mpya za nidhamu.