Mkurugenzi Arsenal aibuka mazoezini kufuatilia mwenendo wa timu

Mkurugenzi Arsenal aibuka mazoezini kufuatilia mwenendo wa timu

LONDON, ENGLAND. KATIKA hali ya kushangaza Mkurugenzi wa ufundi Arsenal anayefahamika kwa jina la Eduardo Daud Gaspar, ameonekana viwanja vya London Colney unaotumika kwa mazoezi ya timu hiyo.

Edu alionekana akiwa mwenye msongo wa mawazo akiwa ameshika tama, akifuatilia mazoezi  ya kujiandaa na mechi ya Ligi Kuu England Jumamosi dhidi ya Burnley.

Arsenal ilipata ushindi wa kwanza msimu huu ilipomenyana na Norwich City, kwa kuichapa bao 1-0 wikiendi iliopita.

Aidha kwa upande wa Edu hakuridhishwa na kiwango cha Arsenal msimu huu, licha ya kufanya usajili wa Ben White, Martin Odegaard na Aaron Ramsdale.

Imeelezwa sababu ya Edu kutinga mazoezini kufuatilia mwenendo mzima wa benchi la ufundi la Arsenal.