Mke mlevi amsumbua Rainford Kalaba

LUSAKA, Zambia KIUNGO wa timu ya taifa ya Zambia, Rainford Kalaba ameshutumiwa na mke wake aliyemuacha kwamba anampiga na pia amemtelekeza mtoto wake. Lakini hata hivyo Kalaba amepinga tuhuma hizo huku akidai mke wake huyo anayeitwa Mwiche anatumia kigezo cha kuzaa naye mtoto kupata fedha na kuzitumia kwa maisha yake ya starehe. Juzi Mwiche alikwenda kwenye ofisi za gazeti la Post la Zambia mjini Kitwe akimtaka rais wa Shirikisho la Soka la Zambia (FAZ), Kalusha Bwalya kuingilia kati ili Kalaba atoe fedha kwa ajili ya kumsaidia mtoto wake mwenye miaka mitano hivi sasa. Akiwa katika ofisi za gazeti hilo la Post, Mwiche alionyesha jinsi alivyoumia usoni akidai kila akiomba fedha za matunzo ya mtoto amekuwa akipigwa na Kalaba na hivyo aliamua kuondoka kwenye nyumba ya Kalaba. "Naamini Kalusha Bwalya anaweza kumuweka chini Kalaba, mimi siombi kitu kwa Kalaba kwa faida yangu, ila nataka Kalaba amsaidie mtoto, huyu ni mtoto wetu, tazama uso wangu, Jumamosi iliyopita nilienda kuomba fedha za matunzo ya mtoto alinipiga, kila mara nikimuomba fedha za matumizi ananipiga, mtoto wetu anasoma shule ya kawaida wakati Kalaba anaandaa sherehe mbalimbali na kustarehe na wachumba zake,"alisema Mwiche. Mwiche anadai amekuwa akimshtaki Kalaba katika kituo cha polisi mjini Kitwe, lakini amekuwa achukuliwi hatua yoyote, anasema alifungua kesi mahakamani, lakini Kalaba alikuwa haendi mahakamani na hakufanywa chochote. "Hivi sasa nimechoka, siku zote nimekuwa namheshimu kwa sababu anajidai anajali na baba bora, wakati timu ya taifa ilipoweka kambi kwenye hoteli ya Michelangelo nilimpigia simu akaniambia niende na mtoto wetu Diego, lakini hakunipa fedha, naomba Kalusha akae na Kalaba ili aweze kuisaidia familia yake,"alisema Mwiche. Alisema,"mtoto huyu nui mto wake, Kalaba hivi sasa amebadilika, Kalaba nayemjua mimi wakatia akichezea Afrisports alipokuwa hana kitu siyo Kalaba ninayemuona hivi sasa, naomba waandishi mnisaidie, nimekuja hapa kwa sababu sina sehemu nyingine ya kwenda." Lakini Kalaba alipotafutwa kuzungumzia suala hilo alisema anatoa fedha nyingi za matunzo ya mto wake ila mke wake huyo amekuwa akitumia vibaya fedha anazompa. "Vyote alivyosema ni uongo, msichana huyo ni mtukutu, natarajia kumpeleka mahakamani ili nipate haki ya kumtunza mwenyewe mtoto wangu na kumaliza tatizo hili, mimi nacheza soka mjini Lubumbashi katika klabu ya TP Mazembe, natuma fedha mara kwa mara ila napata taarifa kwa watu wa nyumbani mjini Kitwe kuwa mtoto wangu hatunzwi vizuri na mama yake,"alisema Kalaba. Alisema,"Mwiche anakunywa sana pombe, amekuwa akitumia fedha ninazomtumia kwa ajili ya mtoto, anakunywa na marafiki zake, ninampatia fedha nyingi kwa ajili ya matunzo ya mtoto, kama anasema sitoi fedha kwa ajili ya mtoto je mtoto huyo amekuwa vipi?," alihoji Kalaba. Kalaba alisema,siku ya Jumamosi alinifuata mjini Ndola na kuniomba fedha, nilimpa Kwacha 1milioni, lakini anamtumia mtoto kupata fedha za kulewa, mimi nataka nimchukue mtoto nikaishi naye DR Congo, lakini Mwiche anakataa kwa sababu anajua hataweza kupiga makelele kama anavyofanya hivi sasa na atakosa fedha."