Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Miaka 14 yamtosha Kyle Walker England, atundika daluga

Muktasari:

  • Walker mwenye umri wa miaka 35 anastaafu baada ya kuitumikia England kwa miaka 14 na ushee tangu alipoichezea kwa mara ya kwanza Novemba 2011 ambapo hadi sasa amecheza idadi ya mechi 96 za timu hiyo.

Beki Kyle Walker ametangaza kustaafu rasmi kuitumikia timu ya taifa ya England baada ya kupoteza nafasi yake katika kikosi cha Meneja Thomas Tuchel miezi michache kabla ya fainali za Kombe la Dunia.

Walker mwenye umri wa miaka 35 anastaafu baada ya kuitumikia England kwa miaka 14 na ushee tangu alipoichezea kwa mara ya kwanza Novemba 2011 ambapo hadi sasa amecheza idadi ya mechi 96 za timu hiyo.

Mara ya mwisho kwa Walker kuitumikia England ilikuwa ni Machi 2025 katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Albania na tangu hapo hakuwemo tena kikosini.

Beki huyo wa Burnley amesema kuwa kuitumikia England imekuwa ni jambo la ufahari kwake.

“Kuichezea England mara zote imekuwa ni heshima kubwa katika maisha yangu ya uchezaji. Kila muda ninapovaa jezi inamaanisha makubwa kwa kwangu na familia yangu.

“Baada ya kujifikiria sana, nahisi kama huu ni muda sahihi kujiweka kando na kuruhusu kizazi kijacho cha wachezaji kuingia. Nina fahari kubwa kwa safari na nashukuru kila meneja, mchezaji mwenzangu na mashabiki ambao wamekuwa sehemu yake.

“Kuwakilisha nchi yako ni jambo kubwa zaidi unaloweza kulifanya katika soka na kumbukumbu zote na England zitabakia kwangu milele,” amesema Walker.

Meneja wa England, Thomas Tuchel amempongeza mchezaji huyo kwa weledi wake na kujitolea kwa hali ya juu.

“Ninajua mashabiki wote wa England wataungana nami kumpongeza Kyle kwa kazi yake kimataifa.

“Kazi ya kimataifa iliyodumu kwa miaka 14 na mashindano matano makubwa ni ujumbe wa kujitolea kwa Kyle. Anaweza kutazama muda wake hapo nyuma akiwa na England kwa fahari kubwa,” amesema Tuchel.