Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mechi ya Argentina, Hispania yafutwa

Muktasari:

  • Finalissima ni mashindano maalumu yanayoandaliwa kwa ushirikiano wa CONMEBOL na UEFA, yakishirikisha mabingwa wa Copa América na UEFA European Championship.

MADRID, HISPANIA: MSIMAMO wa Lionel Messi kuhusu kufutwa kwa mechi ya Finalissima umeibua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki wa soka Hispania na Argentina.

Finalissima ni mashindano maalumu yanayoandaliwa kwa ushirikiano wa CONMEBOL na UEFA, yakishirikisha mabingwa wa Copa América na UEFA European Championship.

Mashindano hayo hufanyika kama mechi moja maalumu na yanafananishwa na Kombe la Intercontinental Cup kwa ngazi ya klabu.

Michuano hiyo ilifanyika mara mbili tu mwaka 1985 na 1993 kabla ya kusitishwa, kisha kurejeshwa tena mwaka 2022 baada ya makubaliano ya ushirikiano kati ya CONMEBOL na UEFA.

Kwa mujibu wa ESPN, nahodha wa Argentina, Messi, alisikitishwa na uamuzi wa kufutwa kwa mechi hiyo kwani aliona ni fursa muhimu ya ushindani kwa timu yake.

Mchezo huo pia ungekuwa nafasi yake ya kwanza kukutana na nyota chipukizi wa Hispania, Lamine Yamal.

Awali mechi hiyo ilikuwa imepangwa kufanyika Machi 27 mjini Doha, Qatar, lakini mipango ilivurugika kutokana na mvutano unaoendelea Mashariki ya Kati.

Baadaye kulikuwa na jitihada za kubadilisha uwanja, lakini UEFA ilisema haikufikia makubaliano na Shirikisho la Soka la Argentina kuhusu mahali pa kuchezwa.

Ripoti zinasema upande wa Argentina haukukubali uwezekano wa mechi hiyo kuchezwa katika Uwanja wa Santiago Bernabéu.

Hata hivyo, licha ya mjadala huo, Messi hakuwa na nafasi katika mazungumzo yaliyofanywa kati ya UEFA, CONMEBOL na waandaaji wa mechi.

Nyota huyo aliamini Finalissima ingekuwa nafasi nyingine ya kuongeza taji akiwa na timu ya taifa ya Argentina.

Taji lake la hivi karibuni alilipata akiwa na Inter Miami baada ya kushinda MLS Cup, Desemba 2025.