Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

McTominay aambiwa ni Barca, Madrid tu

Muktasari:

  • Lakini, staa wa zamani wa Manchester United na Everton, amemtaka kiungo huyo wa Napoli asishawishike kabisa na habari za kurudi igi Kuu England.

NAPLES,  ITALIA: KUNA minongono kwenye klabu za Ligi Kuu England kuhusu shujaa wa Scotland, Scott McTominay, huku Everton ikidaiwa kuwa mstari wa mbele katika msako wa saini ya kiungo huyo.

Lakini, staa wa zamani wa Manchester United na Everton, amemtaka kiungo huyo wa Napoli asishawishike kabisa na habari za kurudi igi Kuu England.

Na badala yake, straika huyo wa zamani wa Ufaransa, Louis Saha alimtaka McTominay alimtaka kufikiria mambo ya juu zaidi, akimtaka kwenda kujiunga na klabu za Hispania, Real Madrid au Barcelona au hata kwa miamba ya Ujerumani, Bayern Munich.

Baada ya kuipaisha Napoli na kunyakua ubingwa wa Serie A msimu uliopita, McTominay aliandika historia mpya kwenye soka la Scotland, wakati alipofunga bao la ticktack kuisaidia timu hiyo kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia 2026 kwa mara ya kwanza baada ya miaka 28. 

Na Saha aliambia punditarena.com:  “Sawa, ni tetesi nzuri, lakini sioni mchezaji wa aina yake kwenda Everton. Nashangaa kusikia uvumi kama huo.

“Sioni hilo likitokea. Nadhani anacheza kwa kiwango bora sana kwa sasa huko Napoli. Kurudi Ligi Kuu England nadhani ni kujirudisha nyuma, hasa kwenda Everton. Itakuwa vyema kama atakwenda Real Madrid au Barcelona, au hata Bayern Munich. Hivyo ndivyo viwango vyake, si kwamba haikosea heshima Everton, lakini, hapaswi kwenda hapo.”