Mbinu bora za kupiga penalti Kombe la Dunia
Muktasari:
- Fainali ya Kombe la Dunia 2022 ilikuwa ya kusisimua sana, ambapo mshindi alipatikana kupitia mikwaju ya penalti baada ya Argentina na Ufaransa kutoka sare ya mabao 3-3. Argentina ilishinda kwa penalti 4-2 na kutwaa ubingwa.
UTUKUFU wa Kombe la Dunia unaweza kuamuliwa kwa mikwaju ya penalti, kwani kadiri hatua za mtoano zilivyoanza, mikwaju hiyo huwa haiwezi kuepukika.
Fainali ya Kombe la Dunia 2022 ilikuwa ya kusisimua sana, ambapo mshindi alipatikana kupitia mikwaju ya penalti baada ya Argentina na Ufaransa kutoka sare ya mabao 3-3. Argentina ilishinda kwa penalti 4-2 na kutwaa ubingwa.
Hata nje ya mikwaju ya penalti ya kuamua mshindi, penalti moja pekee inaweza kuamua matokeo ya mchezo wa Kombe la Dunia. Hivyo, kuwa na mbinu bora ya kupiga penalti ni jambo muhimu. Je, tafiti na takwimu zinatufundisha nini kuhusu mkakati bora wa kupiga penalti?
Piga kwanza, au angalau shinda kura? Moja ya mambo muhimu ambayo timu inaweza kufanya ni kushinda kura ya sarafu kabla ya mikwaju ya penalti kuanza. Utafiti uliochambua mikwaju ya penalti katika mashindano makubwa, ikiwemo Kombe la Dunia, Euro na Fainali ya Ligi England kati ya 1970 na 2003, unaonyesha kuwa timu inayopiga penalti ya kwanza hushinda kwa asilimia 60.5 mara zote.
Katika utafiti mwingine uliofanyika baada ya mabadiliko ya sheria 2003, ambapo mshindi wa kura al-ipewa haki ya kuchagua kupiga kwanza au pili, ilibainika kuwa kushinda kura kulikuwa na faida kubwa zaidi kuliko kupiga kwanza pekee. Takribani asilimia 60 ya timu zilizoshinda kura zilishinda pia mikwaju ya penalti, ikilinganishwa na asilimia 51 ya timu zilizopiga penalti ya kwanza.
UMUHIMU KUKIMBIA KABLA YA KUPIGA
Moja ya tafiti kubwa zaidi iliyochambua zaidi ya penalti 1,700 katika misimu minne ya kuanzia 2015/16 hadi 2018/19, ilichapishwa 2020 katika Jarida la International Journal of Performance Analysis in Sport, ambapo mwandishi mkuu wa utafiti huo, Mikael Jamil, pamoja na wenzake, walilinganisha mbinu mba-limbali za upigaji penalti katika ligi kuu za England, Hispania, Ujerumani na Italia.
Matokeo yalionyesha kuwa mbinu bora hutofautiana kati ya nchi. Kwa mfano, katika Ligi Kuu England mipira iliyopigwa katikati ya goli ilikuwa na uwezekano mkubwa wa kutinga nyavuni. Lakini La Liga nchini Hispania kona za chini kushoto na kulia ndizo zilikuwa maeneo yenye mafanikio makubwa.
Pia walibaini kuwa kukimbia hatua zaidi ya sita kabla ya kupiga penalti kulihusishwa na mafanikio katika ligi zote nne. Isipokuwa Italia, hata kukimbia hatua mbili hadi tano kulionekana kuwa na matokeo ma-zuri. Kukimbia hatua chache sana hakukuonyesha faida yoyote ya maana.
NGUVU DHIDI YA USAHIHI
Utafiti wa 2002 uliobaini penalti chache ulionyesha kuwa mipira yenye nguvu ndogo huokolewa kwa urahisi zaidi, huku ile yenye nguvu kubwa kupita kiasi huwa na uwezekano mkubwa wa kutoka nje. Vilevile nguvu ya wastani, takribani asilimia 75 ya uwezo wa juu wa mchezaji ndiyo ina nafasi kubwa zaidi ya kufunga.
Katika utafiti wa Jamil 2020, penalti zilizopigwa kwa ndani zilihesabiwa kuwa za usahihi, huku zilizopigwa kwa sehemu ya mbele ya kiatu zikihesabiwa kuwa za nguvu. Mbinu zote mbili zilifanikiwa nchini His-pania, Italia na Ujerumani. Hata hivyo, nchini England, usahihi wa kupiga ndiyo ulihusishwa zaidi na mafanikio.
Kwa mara nyingine, tofauti za kimkakati zilionekana, ambapo England na Italia zikionyesha kupendelea usahihi, huku Hispania na Ujerumani zikionyesha kupendelea nguvu ilhali penalti za mtindo wa panenka hazikuonekana kuwa na mafanikio makubwa katika ligi yoyote.
MAHALI PA KUELEKEZA MPIRA
Tafiti nyingi zimechunguza sehemu ya goli inayolengwa na mchezaji ili kubaini kama kuna eneo bora zaidi la kupiga, ambapo matokeo yanaonyesha kuwa kuna uwiano kati ya hatari na faida. Kwa kifupi, mipira inayolenga sehemu za juu za goli ni migumu zaidi kuokolewa lakini pia ina uwezekano mkubwa wa kutoka nje ya goli.
Ndiyo maana wachezaji wengi hupendelea kupiga chini, wakiamini ni afadhali kipa aokoe mpira kuliko kuukosa kabisa mlango wa goli. Mikwaju ya penalti katika Kombe la Dunia 2022 inaunga mkono hoja hiyo, kwani mipira michache ilielekezwa sehemu za juu za goli.
Baadhi ya tafiti pia zinaonyesha kuwa kupiga katikati ya goli unaweza kuwa mkakati mzuri. Utafiti wa 2009 uliotathmini penalti 311 kutoka ligi mbalimbali duniani uligundua kuwa mipira inayopigwa katikati ilikuwa na uwezekano mdogo wa kuokolewa kuliko ile iliyolenga kona.
Kwa upande wa takwimu za Opta zilizoangazia Ligi Kuu ya England zinaonyesha kuwa, penlati za kona ya chini kushoto zina asilimia 77.2 ya mafanikio, huku zile za kona ya chini kulia zikiwa na asilimia 80 ya kufanikiwa, ilhali zinazopigwa katikati juu zikiwa na asilimia 97.8 ya kujaa nyavuni. Penalti zinazopigwa katika chini mara nyingi zina asilimia 80.2 ya kuingia golini.
TABIA ZA MAKIPA
Tafiti kadhaa zimechunguza pia jinsi makipa wanavyofanya uamuzi wakati wa penalti na kutokana na kasi kubwa ya mpira, mara nyingi kipa hawezi kusubiri kuona mpira unaelekea wapi kabla ya kuruka. Badala yake, hulazimika kubashiri kwa kutegemea lugha ya mwili ya mpigaji na historia yake ya upigaji penalti. Hata hivyo, jambo moja limeonekana mara kwa mara katika tafiti nyingi, kwamba makipa kari-bu kila mara huruka kushoto au kulia, ilhali kati ya asilimia 20 hadi 30 ya penalti hupigwa katikati ya goli.
KIPA DHIDI YA MPIGAJI
Uchambuzi wa penalti 286 kutoka ligi mbalimbali duniani ulilinganisha mwelekeo wa mpira na upande ambao kipa aliruka, ambapo watafiti wanaamini kuwa makipa wana kile kinachoitwa upendeleo wa kuchukua hatua (action bias). Yaani, wanapendelea kuonekana wamejitahidi kwa kuruka upande fula-ni, hata kama wamekosea, kuliko kusimama katikati na kuona mpira ukiingia kwenye kona.
Hata hivyo, kuna matukio machache ambapo makipa walibaki katikati na kufanikiwa kuokoa penalti za mtindo wa panenka, kama ilivyofanywa na Andrew “The Grey Wiggle” Redmayne katika fainali ya A-League Men 2019, na Edouard Mendy (Senegal) katika fainali ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) dhidi ya Morocco, Januari, mwaka huu.
KUTOTABIRIKA NDO SILAHA MUHIMU
Ingawa takwimu zinaonyesha kuwa makipa mara nyingi hawawezi kubaki katikati, na hivyo kufanya penalti za katikati kuwa na nafasi nzuri ya kufungwa, wataalamu wa mchezo wa soka wanaeleza kuwa penalti zinategemea pia kanuni za nadharia ya michezo.
Makipa wengi hupewa taarifa kuhusu tabia za wapigaji penalti wa wapinzani wao. Ikiwa wachezaji wote wangeanza kupiga katikati mara nyingi zaidi, makipa wangerekebisha mbinu zao na kuanza ku-baki katikati.
Kwa hiyo, watafiti wanahitimisha kuwa mkakati bora zaidi kwa mpigaji penalti ni kutotabirika. Wachezaji wanapaswa kubadilisha mbinu zao mara kwa mara ili kuwafanya makipa washindwe kutabiri watakakoelekeza mpira.