Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbeumo apenda posti ya mazoezini Man United

Muktasari:

  • Fowadi huyo wa Brentford amekuwa kwenye rada za Man United dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi na ofa mbili za kumhusu zimekataliwa na klabu yake, ikihitaji kulipwa Pauni 60 milioni. Bado anawindwa na miamba hiyo ya Old Trafford wakiamini watanasa saini yake.

LONDON, ENGLAND: STAA Bryan Mbeumo amebonyeza kitufe kilichoandikwa 'like' kwenye posti ya beki wa Manchester United, Leny Yoro, aliyoposti huko kwenye Instagram akithibitisha kurejea mazoezini kitu ambacho mashabiki wamekitafsiri Mcamerooni huyo anataka kutua Old Trafford.

Fowadi huyo wa Brentford amekuwa kwenye rada za Man United dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi na ofa mbili za kumhusu zimekataliwa na klabu yake, ikihitaji kulipwa Pauni 60 milioni. Bado anawindwa na miamba hiyo ya Old Trafford wakiamini watanasa saini yake.

Mbeumo hajataka kuficha kitu kuhusu dhamira yake ya kwenda kuhamia kwenye miamba hiyo ya Ligi Kuu England, ambao wanahitaji kuboresha safu yao ya ushambuliaji ili iwe ya kibabe.

Kitu hicho alichokifanya kwenye Instagram kinachomhusu mchezaji wa Man United kimeibua imani kubwa mchezaji huyo ndoto zake kwa sasa ni kwenda kujiunga na miamba hiyo.

Beki Yoro aliposti ujumbe uliosomeka: "ReUnited" sambamba na picha yake akiwa mazoezini na Mbeumo alikuwa miongoni mwa walioonyeshwa kupendezwa na hilo, wakiwamo mastaa wa Old Trafford, Bruno Fernandes na Diogo Dalot.

Mbeumo atakwenda kuboresha mshahara wake endapo kama atajiunga na Man United na anaripotiwa atalipwa Pauni 200,000 kwa wiki. Makubaliano binafsi hayatakuwa tatizo kabisa endapo kama klabu zitakubaliana juu ya ada, lakini Man United bado haijapeleka ofa ya tatu.

Staa wa kiwango cha juu ambaye Man United imemsajili kwenye dirisha hili ni Mbrazili, Matheus Cunha, aliyemng'oa kutoka Wolves, lakini kocha Amorim bado anamataka Mbeumo, ambaye alifunga mabao 20 msimu uliopita, ikiwamo kufunga dhidi ya Man United.