Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbappe amewaangamiza wenzake wa utotoni

MBAPPE Pict

Muktasari:

  • Mabao ya Kylian Mbappe na Ousmane Dembele yaliihakikishia Les Bleus ushindi huo, huku Mbappe akiendelea kung'ara kwa kufikisha mabao nane katika mashindano hayo na kuongeza asisti moja kwenye bao la pili lililofungwa na Dembele, jambo lililomfanya atangazwe Mchezaji Bora wa Mechi.

UFARANSA imekata tiketi ya kutinga nusu fainali ya Kombe la Dunia 2026 baada ya kuichapa Morocco mabao 2-0 katika mchezo uliokuwa na simulizi ya kipekee iliyowakutanisha Kylian Mbappe na baadhi ya wenzake wa utotoni waliowahi kucheza pamoja katika timu za vijana za Ufaransa.

Mabao ya Kylian Mbappe na Ousmane Dembele yaliihakikishia Les Bleus ushindi huo, huku Mbappe akiendelea kung'ara kwa kufikisha mabao nane katika mashindano hayo na kuongeza asisti moja kwenye bao la pili lililofungwa na Dembele, jambo lililomfanya atangazwe Mchezaji Bora wa Mechi.

Lakini mbali na ushindi huo, mchezo huo uliibua simulizi ya kuvutia kutokana na uwepo wa kiungo Ayoub Bouaddi na beki Issa Diop katika kikosi cha Morocco. Wawili hao waliwahi kucheza pamoja na Mbappe katika timu mbalimbali za vijana za Ufaransa kabla ya kuamua kuichezea Morocco kutokana na asili zao.

MBAP 01

Bouaddi, ambaye alijitahidi kumdhibiti Mbappe kwa muda mrefu wa mchezo, anamfahamu vizuri mshambuliaji huyo wa Real Madrid baada ya kushirikiana naye katika timu za vijana za Ufaransa walipokuwa wakikua kisoka.

Kwa upande wa Diop, aliwahi kucheza sambamba na Mbappe katika kikosi cha Ufaransa chini ya miaka 19 kilichotwaa ubingwa wa Ulaya. Baadaye beki huyo aliamua kubadili uraia wa kimichezo na kuichezea Morocco, akifuata asili ya familia ya mama yake.

Mchezo wa jana ulikuwa wa kwanza kwa Mbappe na Diop kukutana wakiwa upande tofauti wa mataifa. Dakika ya 26, Diop alionekana akizungumza na Mbappe wakati Ufaransa ilipopata penalti, huku beki huyo akionekana kujaribu kumuwekea presha mshambuliaji huyo kabla ya kupiga mpira.

MBAP 02

Mbappe alishindwa kuitumia vyema nafasi hiyo baada ya kupiga penalti dhaifu upande wa kulia wa kipa Yassine Bounou, ambaye aliokoa kirahisi. Kwa kawaida, Mbappe amekuwa na mafanikio makubwa zaidi anapopiga penalti kuelekea upande wa kushoto wa kipa.

Kikosi cha Morocco kilichoshiriki Kombe la Dunia 2026 pia kilikuwa na idadi kubwa ya wachezaji waliozaliwa nchini Ufaransa. Mbali na Bouaddi (Senlis) na Diop (Toulouse), wengine ni Radouane Halhal (Montpellier), Samir El Mourabet (Strasbourg), Neil El Aynaoui (Nancy) na Gessime Yassine (Salon-de-Provence).

Uwepo wa wachezaji hao unaonyesha namna Ufaransa imeendelea kuwa chimbuko la vipaji vingi vinavyozitumikia timu mbalimbali za taifa duniani, huku safari hii Mbappe akiwa ndiye aliyewavunja moyo marafiki zake wa zamani kwa kuwaondoa Morocco katika mbio za kutwaa Kombe la Dunia.