Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbappe afunga friikiki, mashabiki wakataa

Muktasari:

  • Mfaransa huyo alifunga mara mbili wakati Real Madrid ilipoichapa Leganes 3-2 katika mchezo wa La Liga na kuifikia Barcelona kileleni kabla ya wakali hao wa Nou Camp hawajaichapa Girona na kuweka tena pengo la pointi tatu.

MADRID, HISPANIA: SUPASTAA, Kylian Mbappe amefunga bao lake la kwanza kwa mpira wa adhabu, lakini mashabiki wanambishia kwamba hilo halikuwa bao la friikiki.

Mfaransa huyo alifunga mara mbili wakati Real Madrid ilipoichapa Leganes 3-2 katika mchezo wa La Liga na kuifikia Barcelona kileleni kabla ya wakali hao wa Nou Camp hawajaichapa Girona na kuweka tena pengo la pointi tatu.

Bao lake la ushindi Mbappe alifunga kwa frii-kiki, ambapo alifunga kwa shuti matata kabisa lililovuka ukuta na kuingia pembezoni kabisa kwa goli.

Hata hivyo, mashabiki wamedai kwamba hawawezi kulihesabu bao hilo kuwa ni la friikiki, kwa sababu aligusa mpira kwanza kwa Fran Garcia kabla ya kupiga na kufunga. Garcia aligusa mpira kabla ya Mbappe kupiga na kufunga, hivyo haikuwa friikiki kwa mujibu wa mashabiki.

Na mashabiki hao walitumia kurasa zao za mitandao ya X na kuelezea, wakisema: “Nilikuwa sijaona asisti kwenye friikiki.”

Shabiki mwingine alisema: “Ile sio friikiki”.

Shabiki mwingine alisema: “Ile ni aina ya mipigo tunayosema sio ya moja kwa moja. Ni aina ya friikiki ambazo zipo kwenye mchezo wa soka. Mchezaji mwingine anapogusa mpira inahesabika kama asisti na friikiki itahesabika kama pigo lisilokuwa huru. Hivyo, Mbappe bado hajafunga frii-kiki.”