Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Matheus Cunha ameshatua kuwashika

CUNHA Pict

Muktasari:

  • Fowadi huyo wa Kibrazili amesaini mkataba utakaofika tamati Juni 2030 baada ya kutoka Wolves inayoshiriki pia Ligi Kuu England.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United imetangaza ujio wa staa mpya kikosini, Matheus Cunha.

Fowadi huyo wa Kibrazili amesaini mkataba utakaofika tamati Juni 2030 baada ya kutoka Wolves inayoshiriki pia Ligi Kuu England.

Cunha, 26, aliigharimu Man United Pauni 62.5 milioni na atakwenda kulipwa Pauni 200,000 kwa wiki jambo litakalomfanya kushika namba nne kwa wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa kwenye timu.

Staa huyo kwenye utambulisho wake alipiga picha akiwa na jezi za miamba hiyo ya Old Trafford.

Mkurugenzi wa soka wa Man United, Jason Wilcox alisifia usajili wa staa huyo mwenye kipaji kikubwa.

Bosi huyo anaamini Cunha ni mmoja wa wachezaji walionyesha kiwango bora kwenye soka la England msimu uliopita.

Wilcox alisema: “Kumsajili Matheus ilikuwa moja ya vipaumbele vyetu vikubwa kwenye dirisha hili, hivyo tumefurahi kwa kukamilisha usajili huu. Ameonyesha uwezo mkubwa na kufanikiwa kwenye Ligi Kuu England, akionyesha hilo Wolves na kabla ya hapo huko Hispania na Ujerumani.

“Alikuwa na viwango vile ambavyo tunavihitaji kujenga timu yetu yenye nguvu na amekuwa akicheza soka la burudani na lenye ushindani na yupo tayari kwa ajili ya vita ya kupambania mataji.”

Akizungumzia uhamisho wake, Cunha alisema anaamini atakwenda kuwa na msaada mkubwa Old Trafford: “Ni ngumu sana kuelekea kwa maneno kwa jinsi ninavyojisikia kwa kuwa mchezaji wa Man United. Tangu nilipokuwa mtoto Brazil nimekuwa nikiangalia mechi za Ligi Kuu England kwenye televisheni nyumbani kwa bibi yangu, Man United ilikuwa mapenzi yangu na nilikuwa na ndoto za kuvaa jezi nyekundu.

“Naishukuru familia yangu na kila mtu aliyesaidia kutimiza ndoto hizi.”