Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Brazil yaifuata Canada 16 bora Kombe la Dunia

BRAZIL Pict

Muktasari:

  • Brazil ililazimika kucheza kwa nguvu mbele ya Japan iliyocheza kwa nidhamu kubwa ya kiulinzi kabla ya kukata tiketi ya kuendelea kulisaka taji la sita la dunia.

HOUSTON, MAREKANI: TIMU ya Taifa ya Brazil imefuzu hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia 2026, baada ya kuiondoa Japan ikiitandika kwa mabao 2-1 katika mechi mgumu ya hatua ya 32 bora iliyochezwa kwenye Uwanja wa NRG, jijini Houston.

Brazil ililazimika kucheza kwa nguvu mbele ya Japan iliyocheza kwa nidhamu kubwa ya kiulinzi kabla ya kukata tiketi ya kuendelea kulisaka taji la sita la dunia.

Brazil inaungana na Canada iliyofuzu jana baada ya kuitandika Afrika Kusini bao 1-0 na kutinga hatua ya 16 bora.

Baada ya matokeo hayo Brazil sasa itakutana na mshindi kati ya Norway na Ivory Coast kwenye mechi itakayopigwa kesho, Jumatano.

Japan ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 29 la kiungo wake, Kaishu Sano, aliyenufaika na makosa ya Brazil ambao walipoteza mpira katikati ya uwanja. 

BRA 01

Sano aliukaba mpira, akamkwepa Casemiro na kukokota mbele kabla ya kupiga shuti la mguu wa kulia akiwa nje kidogo ya eneo la hatari, mpira uliomshinda kipa Alisson.

Bao hilo lilikuwa la kwanza kwa Sano kwenye mashindano ya Kombe la Dunia na liliipa Japan uongozi baada ya kutumia vyema mashambulizi ya kushtukiza dhidi ya Brazil iliyokuwa ikimiliki mpira kwa kiasi kikubwa.

Brazil ilisawazisha dakika ya 56 kwa bao la Casemiro, aliyefunga kwa kichwa baada ya kupokea krosi iliyopigwa na Gabriel Magalhães upande wa kushoto.

BRA 02

Kabla ya bao hilo, Brazil ilikuwa imeongeza kasi ya mashambulizi kipindi cha pili na kumlazimisha kipa Zion Suzuki kuokoa hatari kadhaa, huku mabeki wa Japan wakiondoa mipira miwili iliyokuwa inakwenda wavuni. 

Hata hivyo, Casemiro aliruka juu ya mabeki wa Japan na kuunganisha krosi hiyo kwa kichwa kilichojaa nguvu na kuisawazishia Brazil mabao 1-1.

Wakati mashabiki wakiamini mechi hiyo imemalizika kwa sare, Gabriel Martinelli akafunga bao la pili dakika za jioni na kuipa Brazil tiketi ya kufuzu.