Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa kibao wawekwa kando kikosi cha FIFPRO

Muktasari:

  • Mastaa watano kutoka kwenye Ligi Kuu England wamepata nafasi ya kuingia kwenye kikosi hicho na kuungana na wakali wengine kadhaa wa La Liga.

LONDON, ENGLAND: SHIRIKISHO la wanasoka wa kulipwa (FIFPRO) limefichua kikosi chake cha kwanza bora huku majina kibao ya wanasoka mastaa yakikosekana.

Mastaa watano kutoka kwenye Ligi Kuu England wamepata nafasi ya kuingia kwenye kikosi hicho na kuungana na wakali wengine kadhaa wa La Liga.

Kipa wa Manchester City, Ederson ametajwa kwenye kikosi hicho, jambo ambalo limeibua maswali kadhaa kutoka kwa mashabiki.

Mabeki wa Real Madrid, Dani Carvajal na Antonio Rudiger wataungana na mkali wa Liverpool, Virgil van Dijk kwenye safu ya ulinzi ya kikosi hicho, huku staa wa Man City, Kevin De Bruyne akiwa kwenye wingi ya kulia na Jude Bellingham wa Los Blancos akiwa upande wa kushoto.

Kiungo wa Man City na mshindi wa Ballon d’Or, Rodri atacheza sambamba na Toni Kroos, ambaye kwa sasa amestaafu soka baada ya kuisaidia Los Blancos kunyakua taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita, watasimama kwenye sehemu ya katikati ya uwanja.

Wakali wawili wa Real Madrid, Kylian Mbappe na Vinicius Jr wataungana na straika wa Man City, Erling Haaland kwenye safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.

Hata hivyo, mashabiki hawakufurahishwa na kikosi hicho kwa sababu kuna mastaa kibao wenye majina makubwa wamekosekana kwenye timu.

Miongoni mwa mastaa hao ni mkali wa Liverpool, Mohamed Salah, wa Chelsea, Cole Palmer, wa Arsenal, William Saliba na wa Barcelona, Lamine Yamal, licha ya kuonyesha kiwango bora kabisa kwenye klabu yake na timu ya taifa ya Hispania.

Shabiki mmoja aliandika kwenye Twitter: “Huu ni utani. Ederson anafanya nini humu?

Mwingine aliongeza: “Mbappe hafai hata kwenye wingi ya kulia, hivi wamefanya kitu gani kumweka kando Salah.”

Shabiki wa tatu aliandika: “Lamine Yamal amedhulumiwa.”

Mwingine aliandika: “Hivi kuna kitu kingine cha ziada Palmer anapaswa kukithibitisha?” Na shabiki mwingine alihoji: “Saliba yupo wapi?”