Maskini Mr Ibu kaondoka na kipaji chake

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Tangu mwishoni mwa mwaka jana inaelezwa hali ya kiafya ya mchekeshaji huyo aliyeshiriki na kuigiza filamu zaidi ya 200 ilianza kuyumba kabla ya hivi karibuni kubadilika, ambapo amefariki dunia akiwa hospitali.

MWIGIZAJI na mchekeshaji maarufu wa filamu za Kinaijeria, John Okafor 'Mr Ibu' amefariki dunia jana Jumamosi wakati akipatiwa matibabu hospitalini jijini Lagos, Nigeria.

Taarifa kutoka nchini humo  zilizothibitishwa na Raia wa Chama cha Waigizaji wa Nigeria, Emeka Rollas zinasema kuwa Mr Ibu alikumbwa na mauti hayo katika hospitali ya Evercare iliyopo Lekki jijini Lagos baada ya kuwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) kwa siku chache zilizopita kutokana na kupatwa na shambulio la moyo.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Mr Ibu aliyetamba na filamu zaidi ya 200 zilizotikisa nchini humo na barani Afrika kwa ujumla, inaelezwa amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 62.

Rais wa Waigizaji wa Nigeria,  Rollas ndiye aliyetoa taarifa ya msiba huo usiku wa jana kupitia akaunti yake ya Instagram, akielezwa kuwa Mr Ibu alipatwa na shinikizo la moyo na kufariki hospitali.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

“Mr. Ibu amefariki dunia kwa shambulio la moyo kwa mujibu wa meneja wake, Don Single Nwuzor. Kwa masikitiko makubwa napenda kutangaza taarifa hii ya huzuni kwamba Mr Ibu hatunaye. Roho yake ipumzike kwa amani," aliandika Rollas.

Tangu mwishoni mwa mwaka jana inaelezwa hali ya kiafya ya mchekeshaji huyo aliyeshiriki na kuigiza filamu zaidi ya 200 ilianza kuyumba kabla ya hivi karibuni kubadilika, ambapo amefariki dunia akiwa hospitali.

Novemba, mwaka jana familia ya Mr Ibu ilitangaza juu ya mwigizaji huyo kukatwa mguu kwa sababu za kitabibu.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Katika taarifa hiyo iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ilieleza, Mr Ibu alikuwa akijiandaa kufanyiwa upasuaji kabla ya kuelezwa ilikuwa lazima akatwe mguu huo ili kuokoa uhai  na familia iliridhia.

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali kutoka Nigeria, inaelezwa kwamba kwa nyakati tofauti wakati akiugua aliomba achangiwe kwa ajili ya kugharimia matibabu yake, ambapo baadhi ya taasisi na watu binafsi walifanya hivyo.

Enzi za uhai wake Mr Ibu aliyezaliwa Oktoba 17, 1961 na kuoa mara mbili akijaliwa kupata zaidi ya watoto 10 alitamba kupitia kazi mbalimbali za filamu za Nollywood zikiwamo Aki and Pawpaw, Keziah, 9 Wives na Mr Ibu in London.

Filamu iliyomtambulisha zaidi kwa mashabiki wa filamu za Nollywood ni Mr Ibu (2004), Mr Ibu 2 (2005), Mr Ibu and His Son, Coffin Producers, Husband Suppliers na International Players.

Pia aliwahi kujihusisha na masuala ya muziki ambapo Oktoba 15, 2020 alirekodi nyimbo mbili za 'This Girl' na 'Do You Know'.