Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashabiki Man City waanza mbwembwe

Muktasari:

  • Chelsea walikubali kichapo cha aibu nyumbani katika Ligi Kuu England, ambacho kilikiacha kikosi cha Kocha Liam Rosenior kikiugulia maumivu ambayo yameanza kupunguza uwezekano wa kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwakani, kwani kinashika nafasi ya sita kikiwa na pointi 48 nyuma ya Liverpool yenye alama 52.

LONDON, CHELSEA: ACHANA na matokeo ya uwanjani Stanford Bridge, juzi, katika kichapo walichokipata wenyeji, Chelsea kutoka kwa Manchester City cha mabao 0-3, lakini kulikuwa na vaibu lingine nyuma lililoanzishwa na mashabiki wa kikosi hicho cha Pep Guardiola na kuliendeleza hata baada ya kutoka uwanjani.

Chelsea walikubali kichapo cha aibu nyumbani katika Ligi Kuu England, ambacho kilikiacha kikosi cha Kocha Liam Rosenior kikiugulia maumivu ambayo yameanza kupunguza uwezekano wa kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwakani, kwani kinashika nafasi ya sita kikiwa na pointi 48 nyuma ya Liverpool yenye alama 52.

Lakini, katika ushindi huo upande wa Man City, mashabiki walianza kusherehea namna kikosi hicho kinavyoanza kuufukuzia ubingwa baada ya wapinzani wao wakubwa, Arsenal, kupoteza Jumamosi kwa mabao 2-1.

Kwa mashabiki wa Man City waliokuwa Darajani walionekana wakijipongeza kwa vileo vya aina mbalimbali, huku wakiuhanikiza uwanja kwa shamrashamra kana kwamba tayari wameshabeba ubingwa na hata walipotoka ndani ya uwanja waliendelea kufanya hivyo kwenye baa zilizopo jirani.

Kinachowapa matumaini ya ubingwa mashabiki hao ni alama sita zinazowatofautisha na Arsenal, ambapo kikosi chao kina pointi 64 huku wapinzani wao wakiwa nazo 70 sawa na michezo miwiliwakiamini mchezo ujao wanaowakaribisha Arsenal watashinda na kupunguza tofauti iliyopo, kisha wataenda Burnley na Everton kuchukua pointi. 

Ingawa hilo linaweza kuwa suala gumu, lakini ubora ambao kikosi chao kimeanza kuupata katika michezo ya karibuni unaashiria nyota njema mbele ya safari iwapo hakutakuwa na kupoteza alama kizembe wakiwa na michezo saba mkononi mmoja zaidi ya wapinzani wao hao.

Arsenal wamepoteza mechi tatu kati ya nne zilizopita katika mashindano yote, na wanaonekana kuanza kuonyesha presha. Kikosi cha Mikel Arteta kimekuwa cha pili katika misimu mitatu iliyopita na kumaliza tena nafasi hiyo kwa mara ya nne mfululizo itakuwa maumivu makubwa.

Pia Arsenal wanajua mchezo ujao wa ligi unaweza kuamua msimu, kwani watasafiri kwenda kukutana na City Jumapili ijayo. City waliwahi kuwakaribisha Arsenal katika mazingira kama haya mwishoni mwa msimu wa 2022/23 na Kevin De Bruyne, John Stones na Erling Haaland walifunga mabao na kuwapoteza wapinzani wao hao.

Katika mechi ya juzi Man City waliichapa Chelsea kwa mabao 3-0 yaliyotupiwa nyavuni na Nico O'Reilly, Marc Guehi na Jeremy Doku. Mara ya mwisho walipokutana mwezi uliopita, ambapo City walishinda 2-0 katika fainali ya Carabao.


ARSENAL SITA ZA MWISHO EPL

April 19 vs Man City         (ugenini)

April 25 vs Newcastle Utd             (nyumbani)

May 2 vs Fulham                              (nyumbani)

May 10 vs West Ham United       (ugenini)

May 17 vs Burnley                           (nyumbani)

May 24 vs Crystal Palace               (ugenini)


MAN CITY SABA ZA MWISHO EPL

April 19 vs Arsenal                           (nyumbani)

April 22 vs Burnley                           (ugenini)

May 4 vs Everton                             (ugenini)

May 9 vs Brentford                         (nyumbani)

May 17 vs Bournemouth              (ugenini)

May 24 vs Aston Villa      (nyumbani)

Itapangiwa vs Crystal Palace        (nyumbani)