Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashabiki Mali waishangilia Walibya

Mashabiki wa Mali wiinua picha za kiongozi wa Libya juu

BAMAKO, Mali MAELFU ya mashabiki wa soka wa Mali, juzi waliishangiliwa Libya kwa nguvu ilipokuwa ikicheza na Comoro katika mechi ya kuwania kufuzu Fainali za Afrika 2012. Mechi hiyo ilifanyika kwenye mji wa Bamako nchini Mali kutokana na uwepo wa usalama mdogo nchini Libya. Zaidi ya mashabiki 20,000 wa Mali walikuwa na mabango yenye picha za kiongozi wa Libya huku wakiwa na mabango yanayopinga hatua za mataifa ya magharibi kuivamia Libya. Katika mchezo huo, Libya ilishinda mabao 3-0. "Mashabiki wa Mali walitupa nguvu sana," alisema nahodha wa Libya, Tariq Ibrahim al-Tayib alipozungumza na BBC baada ya mchezo huo. Mwandishi wa habari anayeishi kwenye mji wa Bamako, Martin Vogl alisema serikali ya Mali na Libya zina uhusiano wa karibu na kiongozi wake, Muammar Gaddafi kwani wamekuwa wakiisaidia nchi hiyo katika nyanja mbalimbali. Baada ya mchezo huo kumalizika, mashabiki walikuwa wakipiga kelele: "Gaddafi! Gaddafi," alisema. Tayib alisema kuwa wachezaji wengi wameshindwa kujiunga na timu hiyo kwa kuwa wako Benghazi, mji wenye mgogoro mkubwa kati ya waasi na wanajeshi wa serikali ya Gaddafi. Hata hivyo alisema, hakuna mgawanyiko wa kisiasa kwenye suala la timu. "Timu yote ni ya Muammar Gaddafi," alisema. "Tunawapa ushindi huu wananchi wote wa Libya ambao wameangamia kwa njia moja ama nyingine," aliiambia Associated Press.