Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashabiki England wasusia mechi ya kirafiki Marekani

MASHABIKI Pict

Muktasari:

  • Katika mchezo wao wa kwanza wa maandalizi ya Kombe la Dunia dhidi ya New Zealand (All Whites) utakaopigwa Juni 6, takriban viti 50,000 vinatarajiwa kuwa wazi.

Nahodha wa timu ya taifa ya England, Harry Kane na wachezaji wenzake wanakabiliwa na uwezekano wa kucheza mbele ya uwanja usio na mashabiki wengi nchini Marekani wiki ijayo.

Katika mchezo wao wa kwanza wa maandalizi ya Kombe la Dunia dhidi ya New Zealand (All Whites) utakaopigwa Juni 6, takriban viti 50,000 vinatarajiwa kuwa wazi.

Mchezo huo utafanyika kwenye Uwanja wa Raymond James mjini Tampa, Florida, unaochukua mashabiki 69,000, lakini hadi sasa ni tiketi 13,000 tu ndizo zilizouzwa.

MASHA 02

Hali hii ya mauzo madogo ya tiketi imejitokeza licha ya uwepo wa takriban raia 400,000 wa England wanaoishi katika jimbo la Florida.

Kati ya nafasi 3,776 zilizotengwa kwa ajili ya wanachama rasmi wa klabu ya wasafiri wanaoshabikia England (England Supporters Travel Club), ni mashabiki 1,500 tu wanunua tiketi hadi sasa.

Tiketi ya bei ya chini kabisa kwenye mchezo huo inagharimu pauni 54 (Sh190,082), kiwango ambacho Chama cha Soka cha England (FA) kinasisitiza kuwa ni cha kawaida kwa viwango vya michezo nchini Marekani, ingawa tiketi za mechi kati ya Marekani na Senegal zinapatikana kwa pauni 29 (Sh102,081).

MASHA 03

Baada ya mchezo huo wa kwanza, kikosi cha England kinachonolewa na kocha Thomas Tuchel kitasafiri hadi Orlando kucheza mechi ya pili ya kirafiki dhidi ya Costa Rica Juni 10.

Mchezo huu unaonekana kuvutia mashabiki wengi zaidi ambapo tiketi 12,000 tayari zimeuzwa katika Uwanja wa Inter&Co unaochukua watu 25,500, huku idadi kubwa ya mashabiki ikichangiwa na ukweli kwamba raia wa Costa Rica wanajumuisha asilimia 16 ya wakazi wa eneo hilo.

Baada ya hapo, England itacheza mechi nyingine ya maandalizi dhidi ya Ujerumani ambapo tiketi zake zinauzwa kwa bei ya juu zaidi, zikianzia pauni 101 (Sh355,524) hadi pauni 661(Sh2.3 milioni).

MASHA 01

Tofauti na mechi hizo za kirafiki, mahitaji ya tiketi za mechi halisi za Kombe la Dunia ni makubwa sana. Zaidi ya mashabiki rasmi 3,000 wa England wamethibitisha tiketi zao kwa ajili ya mechi za makundi zitakazopigwa Dallas, Boston, na New Jersey.

Shirikisho la Soka ulimwenguni (FIFA) limeripoti kuwa tiketi milioni 5 kati ya milioni 6 zilizotengwa kwa ajili ya michezo yote 104 ya Kombe la Dunia nchini Marekani, Canada, na Mexico tayari zimeshanunuliwa.

Kikosi cha England kinatarajiwa kusafiri kwa pamoja Juni 1 kuelekea kambi yao ya maandalizi huko Palm Beach, Florida, isipokuwa wachezaji wa Arsenal na Crystal Palace wanaokabiliwa na fainali mbili za Ulaya.

Baada ya kukamilisha mechi zote za kirafiki, timu hiyo itahamia kwenye kituo chao cha kudumu huko Kansas City. England itafungua rasmi kampeni yake ya kuwania Kombe la Dunia dhidi ya Croatia Juni 17 huko Texas, kabla ya kumenyana na Ghana pamoja na Panama.