Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Marie-Louise Eta kocha wa Union Berlin, aandika historia Bundesliga

Muktasari:

  • Klabu hiyo ya mji mkuu wa Ujerumani ilimfuta kazi Steffen Baumgart baada ya kupoteza kwa mabao 3-1 katika Mechi ya 31, na kufanya uamuzi ambao haujawahi kushuhudiwa katika soka la Ujerumani.

BERLIN, UJERUMANI: UNION Berlin imemteua Marie-Louise Eta kuwa kocha hadi mwisho wa msimu kufuatia kipigo dhidi ya Heidenheim, ambapo anakuwa kocha wa kwanza mwanamke kufundisha timu ya Ligi Kuu Ujerumani (Bundesliga) kwa wanaume. 

Klabu hiyo ya mji mkuu wa Ujerumani ilimfuta kazi Steffen Baumgart baada ya kupoteza kwa mabao 3-1 katika Mechi ya 31, na kufanya uamuzi ambao haujawahi kushuhudiwa katika soka la Ujerumani.

Timu hiyo ya Berlin ilithibitisha uteuzi huo ikiwa na lengo la kuhakikisha inabaki ligi kuu, ambapo zikiwa zimebaki mechi tatu kabla ya msimu kumalizika, Union ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi 31, pointi sita juu ya nafasi za kushuka daraja moja kwa moja. Ingawa kuna pengo la alama, bado kuna presha kubwa ya kubaki na klabu imechagua suluhisho la haraka kutoka kwa mtu anayeijua vyema.

Eta alikuwa sehemu ya mfumo wa kiufundi wa Union Berlin na hadi sasa alikuwa akiifundisha timu ya vijana ya U19. Amejijengea nafasi ndani ya klabu hiyo kwa miaka kadhaa, na uongozi unaamini kuwa uelewa wake wa mazingira ya klabu unaweza kuwa muhimu katika kipindi hiki cha mwisho ambacho timu inahitaji utulivu ili kujinusuru kushuka daraja.

Uteuzi huo pia unakuja katika kipindi cha maisha yake ya ukocha, kwani Aprili 3, mwaka huu Union Berlin walitangaza kuwa atakuwa kocha mkuu wa timu yao ya wanawake kuanzia msimu ujao, lakini sasa atachukua jukumu la timu ya wanaume mara moja hadi mwisho wa msimu.

Baada ya kuteuliwa, Eta alisema: “Ninafurahi klabu imenikabidhi jukumu hili gumu. Moja ya nguvu za Union imekuwa ni umoja wetu katika nyakati kama hizi. Ninaamini pamoja na timu tutapata pointi muhimu.”

Mechi yake ya kwanza itakuwa katika mazingira yenye presha kubwa ya ushindani Jumamosi ijayo watakapoikaribisha Wolfsburg inayoshika nafasi ya pili kutoka mkiani katika msimamo wa Bundesliga.