Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maresca ruksa kubadili kikosi

MARESCA Pict

Muktasari:

  • Chelsea ilitangulia kufunga bao kwenye mechi hiyo, kisha ikajikuta ikiwa nyuma kwa mabao 2-1 kabla ya Alejandro Garnacho kuisawazishia kwenye kipindi cha pili.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Chelsea, Enzo Maresca amepewa ruhusa na mabosi wake kuendelea kuwapa nafasi ya kucheza mastaa wake kwa kubadilibadili kikosi licha ya kwamba jambo hilo liliifanya timu hiyo kupata sare dhidi ya Qarabag kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, Jumatano iliyopita.

Chelsea ilitangulia kufunga bao kwenye mechi hiyo, kisha ikajikuta ikiwa nyuma kwa mabao 2-1 kabla ya Alejandro Garnacho kuisawazishia kwenye kipindi cha pili.

Katika mechi hiyo, kocha Maresca alifanya mabadiliko ya wachezaji saba katika mechi ya tano mfululizo zikiwamo za hivi karibuni ambazo Chelsea ilicheza kwa kiwango cha hovyo.

Chelsea imefanya mabadiliko ya wachezaji mara 85 msimu huu, mara 16 zaidi ya Liverpool.

Vinara wa Ligi Kuu England, Arsenal wanashika nafasi ya tatu kwa kubadilisha wachezaji mara nyingi, wakifanya hivyo mara 67. Baadhi ya mabadiliko hayo yalichagizwa na wachezaji kuwa majeruhi au kutumikia adhabu, lakini mengine ni uamuzi wa kocha.

Lakini, mabosi wa Chelsea kuanzia kwa wamiliki wake, wakurugenzi na benchi la ufundi wanaunga mkono jambo hilo la kubadili kikosi mara kwa mara ili kuendana na ratiba ya mechi nyingi.

Tangu mapumziko ya ligi kupisha mechi za timu za taifa yalipopita, Chelsea imecheza mechi 11 katika michuano yote kabla ya mwaka huu kufika mwisho ikiwa ni ndani ya wiki nne na nusu.

Maresca, ambaye alishinda taji la UEFA Conference League na Kombe la Dunia la Klabu katika msimu wake wa kwanza huko Stamford Bridge, hayupo kwenye presha yoyote ya kibarua chake kuwa hatarini, akiaminiwa na mabosi wake ili kuleta mafanikio makubwa.

Chelsea kwa sasa inashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu England na nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.