Marekani yashinda tena, ikiichapa Australia
Muktasari:
- Dakika 11 tu zikatosha kuwapa bao la kuongoza Marekani, ikinufaika na makosa ya beki wa Australia Cameron Burgess wakati akipambana kuidhibiti shambulizi la wenyeji.
Marekani imeendelea kuonyesha ukomavu, ikishinda mchezo wake wa pili mfululizo wa Makundi ya Kombe la Dunia, ikiichapa Australia kwa mabao 1-0.
Dakika 11 tu zikatosha kuwapa bao la kuongoza Marekani, ikinufaika na makosa ya beki wa Australia Cameron Burgess wakati akipambana kuidhibiti shambulizi la wenyeji.
Beki Alex Freeman akaipa bao la pili Marekani dakika ya 43, akimalizia kwa kichwa mpira uliopanguliwa na kipa wa Australia Patrick Beach, baada ya shambulizi zuri la shuti kali
Marekani ilitawala vizuri dakika 45 za kwanza ikienda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao hayo 2-0 dhidi ya Australia.
Kipindi cha pili kikaendelea kwa timu zote kujaribu kutengeneza nafasi Kila moja ikitengeneza mashuti mawili yaliyolenga lango.
Mpaka mwisho wa mchezo huo Marekani ikatoka na ushindi huo wa mabao 2-0, iliweka uhakika wa kufuzu hatua inayofuata, ikishinda mechi ya pili baada ya awali kupata ushindi mkubwa wa mabao 4-1 dhidi ya Paraguay.
Ushindi huo unaifanya Marekani kuendelea kuongoza kundi lake D ikifikisha pointi sita huku Australia ambayo mchezo wa kwanza iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Uturuki, ikisalia nafasi ya pili wakati Paraguay na Uturuki zikiwa hazina pointi yoyote.