Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United yafuta cheo cha mkurugenzi wa michezo

Muktasari:

  • Bilionea mmiliki wa klabu hiyo ya Old Trafford, Sir Jim Ratcliffe amemfuta kazi Ashworth baada ya kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa Nottingham Forest uwanjani Old Trafford, Jumamosi iliyopita.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United imeamua kukifuta cheo cha mkurugenzi wa michezo baada ya kufeli kwenye jaribio lao la kumtumia Dan Ashworth.

Bilionea mmiliki wa klabu hiyo ya Old Trafford, Sir Jim Ratcliffe amemfuta kazi Ashworth baada ya kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa Nottingham Forest uwanjani Old Trafford, Jumamosi iliyopita.

Ashworth, sasa amekuwa kwenye mawindo ya klabu ya Arsenal ikitaka huduma yake, lakini huko Man United alikuwa mkurugenzi wa michezo wa kwanza.

Lakini, amefutwa kazi baada ya miezi mitano tu  — huku cheo hicho sasa kikibaki kuwa historia.

Bilionea Ratcliffe sasa ameamua msaidizi wake kwenye kampuni ya Ineos, Sir Dave Brailsford, mkurugenzi mtendaji mkuu wa Man United, Omar Berrada na mkurugenzi wa ufundi, Jason Wilcox watagawana majukumu yaliyokuwa yakifanywa na mkurugenzi wa michezo.

Ashworth, 53, alilazimika kuondoka Old Trafford baada ya kushindwa kwenye vita ya madaraka na aliyekuwa mtendaji mkuu wa zamani wa Man City, Berrada.

Wawili hao walipishana lugha kwenye namna ya kuiongoza klabu hiyo kurejea kwenye makali yake kwenye soka la England. Lakini, Ashworth, ambaye aliwahi kufanya kazi Newcastle, Brighton, West Brom na kwenye Chama cha soka cha England, anaweza kupata dili jingine litakalomrudisha mzigoni haraka.

Arsenal inamtazama kama mtu anayeweza kwenda kuchukua nafasi ya Edu ya mkurugenzi wa michezo huko Emirates. Ashworth amekuwa na urafiki wa karibuni na mkurugenzi wa Arsenal, Richard Garlick, ambaye ndiye anayesimamia msako wa mkurugenzi wa michezo mpya. Wawili hao walifanya kazi pamoja West Brom kwa kipindi cha miaka mitatu. Garlick alikuwa mkurugenzi wa sheria The Hawthorns na alikuwa akifanya kazi chini ya Ashworth.

Everton nayo inapiga hesabu za kumchukua Ashworth wakati huu ikisubiri kampuni ya The Friedkin Group kuichukua jumla klabu hiyo.

Kingine kinachoelezwa ni Ashworth hakuunga mkono sana uteuzi wa kocha mpya wa Man United, Ruben Amorim.