Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United waandaa mkakati mpya kumshawishi Anderson

Muktasari:

  • Anderson ameibuka kuwa mmoja wa viungo wanaovutia zaidi kwa sasa kutokana na kiwango chake bora alichoonyesha msimu huu kiasi cha vigogo wa England kupigana vikumbo kutaka kumsajili.

MANCHESTER United imepanga kutumia wachezaji wao raia wa England waliopo timu ya taifa ili kumshawishi kiungo wa Nottingham Forest, Elliot Anderson, 23, kujiunga nao dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Anderson ameibuka kuwa mmoja wa viungo wanaovutia zaidi kwa sasa kutokana na kiwango chake bora alichoonyesha msimu huu kiasi cha vigogo wa England kupigana vikumbo kutaka kumsajili.

Man United inaamini uwepo wa wachezaji wa England katika kikosi chao unaweza kuwa faida katika kumshawishi nyota huyo watakapokuwa kuwa naye katika kambi ya timu ya taifa kuelekea michuano ya Kombe la Dunia.

Man United inakumbana na upinzani mkali kutoka kwa majirani zao Man City ambao pia wanahitaji huduma ya fundi huyu, wakiwa tayari kutoa hadi Pauni 70 milioni ili kufanikisha mchakato.

Mkataba wa Elliot ambaye moja ya sharti la kujiunga na timu yoyote kwa msimu ujao ni kuwa iwe inacheza Ligi ya Mabingwa Ulaya unamalizika mwaka 2029.

Staa huyu tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 41 za michuano yote na kufunga mabao mawili.


Anthony Gordon

BAYERN Munich imeonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Newcastle United na timu ya taifa ya England, Anthony Gordon, 25, dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Nyota huyo ambaye pia anafuatiliwa na Arsenal na baadhi ya timu za England, amekuwa katika rada za vigogo mbalimbali Ulaya kutokana na uwezo wake mkubwa aliouonyesha akiwa na Newcastle.

Mabosi wa Newcastle wanadaiwa kuhitaji takribani Pauni 100 milioni ili kumuuza na hawapo tayari kupunguza bei hiyo.


Yankuba Minteh

LIVERPOOL inamwangalia  winga wa Brighton na Gambia, Yankuba Minteh, 21, kama mbadala wa muda mrefu wa staa wao Mohamed Salah, 33, ambaye anatarajiwa kuondoka dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Minteh ana uhusiano mzuri na Kocha wa Liverpool, Arne Slot, ambaye amewahi kufanya naye kazi pamoja akiwa Feyenoord. Mazungumzo bado yanaendelea ingawa mwanga wa kufikia mwafaka unaonekana kuwa karibu. Mkataba wa Minteh unatarajiwa kumalizika mwaka 2029.

Oscar Mingueza

ARSENAL na Manchester City zimejiunga na Aston Villa katika mbio za kuwania saini ya beki wa Real Betis, Oscar Mingueza, 26. Mingueza, ambaye ana uwezo wa kucheza beki wa kati na pembeni, ameikuwa chaguo linalovutia zaidi kwa klabu hizo za England ambazo zimekuwa zikituma maskauti wake kumtazama tangu kuanza kwa msimu huu. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu. Tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 38 za michuano yote na kufunga bao moja.


Danilho Doekhi

ASTON Villa  na Leeds United zimeingia katika mbio za kuiwania saini ya beki wa  FC Union Berlin, Danilho Doekhi, 27, kuelekea dirisha la majira ya kiangazi. Beki huyo wa kimataifa wa Uholanzi pia anafuatiliwa na Besiktas ya Uturuki ambayo inatajwa kuwa katika mazungumzo na wawakilishi wake. Doekhi ameonyesha kiwango bora katika  Bundesliga na anaonekana kutamani zaidi kwenda Villa licha ya timu nyingi zinazomhitaji.


Arthur Vermeeren

TOTTENHAM Hotspur  inamfuatilia kwa karibu kiungo wa RB Leipzig, Arthur Vermeeren, 21, na inapanga kutuma ofa ya kumsajili dirisha la majira ya kiangazi. Nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji alipata uzoefu wa kutosha alipokuwa kwa mkopo Olympique de Marseille na alifanya kazi chini ya Kocha Roberto De Zerbi. Vermeeren anatajwa kuwa mmoja wa viungo vijana wenye kipaji kikubwa Ulaya na amekuwa mmoja kati ya mastaa wa kwanza kupendekezwa na De Zerbi.


Nico Schlotterbeck

REAL Madrid bado ina mpango wa kumsajili beki wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Ujerumani, Nico Schlotterbeck, 26, licha ya mchezaji huyo kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia viunga vya Signal Iduna Park. Ripoti zinaeleza Madrid inamwangalia Schlotterbeck kama sehemu ya mipango yao ya kuimarisha safu ya ulinzi ikiamini atadumu kwa muda mrefu. Hata hivyo, Dortmund haipo tayari kumwachia kirahisi.


Marco Palestra

LIVERPOOL bado inaendelea kufanya mazungumzo na wawakilishi wa beki wa kimataifa wa Italia, Marco Palestra, 21, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo katika Cagliari Calcio akitokea Atalanta. Palestra  ambaye anacheza kama beki wa kulia ameendelea kuonyesha kiwango bora kutokana kwa msimu huu hali iliyowavutia maskauti wengi wa timu kubwa za Ulaya ambao wamekuwa Italia kumtazama staa huyo akicheza katika mechi kadhaa. Hadi sasa haijajulikana ikiwa Atalanta itaamua kumuuza au itahitaji kuendelea kuwa naye na kumtumia.