Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United kupiga chini nyota 13, Rashford, Casemiro watajwa

MAN UTD Pict

Muktasari:

  • Aidha, baadhi ya wachezaji kutoka kwenye akademi akiwemo Dan Gore ambaye mkataba wake unaisha, pamoja na Toby Collyer na Tyler Fredricson,. wote wanatarajiwa kuondoka.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United inajiandaa kufanya mabadiliko makubwa ya kikosi msimu huu wa kiangazi na jumla ya wachezaji  13 wanatarajiwa kuondoka.

Klabu hiyo iko kwenye kipindi muhimu, ikitathmini nani atakuwa kocha wa kudumu baada ya kazi ya muda ya Michael Carrick, ambaye anakaribia kuiwezesha timu kumaliza katika nafasi tano za juu.

Iwapo Carrick atapewa nafasi hiyo, atakabiliwa na kazi kubwa ya kuijenga upya kwa ajili ya msimu ujao. Msimu uliopita, Man United ilifanya usajili wa washambuliaji Bryan Mbeumo, Matheus Cunha na Benjamin Sesko, lakini walishindwa kuongeza kiungo mpya katika maeneo wanayocheza  kwa Casemiro na Kobbie Mainoo.

Casemiro anatarajiwa kuondoka bure mwishoni mwa msimu na moja kati ya kazi ambayo imekuwa ikifanya kwa sasa ni kufanya mzungumzo na wawakilishi wa viungo wanaoweza kuziba pengo lake.

Kwa mujibu wa ripoti, mbali ya Casemiro, nyota kadhaa pia wako mbioni kuondoka ikiwa pamoja na Marcus Rashford ambaye anatarajiwa kuuzwa baada ya kung’ara kwa mkopo akiwa Barcelona.

Vilevile, Jadon Sancho, Rasmus Hojlund na Andre Onana ambao wanacheza kwa mkopo sehemu mbalimabali nao wanatarajiwa kuondoka mwisho wa msimu. Makipa Altay Bayındır na Radek Vítek pia mustakabali wao hauko wazi.

Kwa upande wa mabeki, Tyrell Malacia naye anatarajiwa kuondoka kama ilivyo kwa kiungo  Manuel Ugarte ambaye amekosa nafasi ya kucheza tangu kuwasili kwa Carrick.

Mshambuliaji Joshua Zirkzee pia anaripotiwa kutoridhishwa na muda mdogo wa kucheza anaopewa, hivyo naye anataka kuondoka.

Aidha, baadhi ya wachezaji kutoka kwenye akademi akiwemo Dan Gore ambaye mkataba wake unaisha, pamoja na Toby Collyer na Tyler Fredricson,. wote wanatarajiwa kuondoka.