Man United imempa presha Carlos Baleba
Muktasari:
- Kiungo huyo wa Cameroon amekuwa na panda shuka kwenye msimu huu wa 2025-26, ambapo Baleba, 21, ametolewa mara 14 katika mechi za timu hiyo kwa msimu huu.
LONDON, ENGLAND: KIUNGO wa Brighton, Carlos Baleba amekiri kwamba tetesi za kutakiwa na Manchester United zilimfanya kuwa na presha kubwa na kumfanya aanze msimu kwa kiwango chenye wasiwasi.
Kiungo huyo wa Cameroon amekuwa na panda shuka kwenye msimu huu wa 2025-26, ambapo Baleba, 21, ametolewa mara 14 katika mechi za timu hiyo kwa msimu huu.
Mashabiki wa Brighton walidai kwamba kiwango cha Baleba kilishuka kutokana na presha iliyotokana na kufeli kwa uhamisho wake wa kwenda kujiunga na Man United kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi.
Akizungumza baada ya kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Liverpool, Jumapili iliyopita, Baleba alisema: “Madai ya kwamba uhamisho ule ulikuwa na athari hasi kwangu si kweli, isipokuwa iliongeza presha kubwa katika maisha yangu.
“Nilipoanza msimu huu, nilitaka kuonyesha kwamba kiwango changu kipo kama msimu uliopita. Kila siku nilijaribu kupambana sana ili kurudi kwenye viwango vyangu. Hilo lilinifanya kuwa na presha kubwa.”
Baleba atakwenda kujiunga na kikosi cha Cameroon kwa ajili ya mashindano ya Afcon 2025 yatakayoanza Desemba 21 hadi Januari 18. Man United ipo kwenye nafasi ya kunasa saini ya mkali huyo endapo kama itakamatia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao na huenda ikapambana kumsajili kwenye dirisha la Januari ili akaisaidie harakati.
Baleba ni miongoni mwa viungo wanaosakwa na Man United sambamba na staa wa Nottingham Forest, Elliot Anderson na Adam Wharton wa Crystal Palace.