Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man City inavyoipa Arsenal presha ya ubingwa

Muktasari:

  • Swali hilo lilijibiwa siku ya Jumapili, wakati kikosi cha Pep Guardiola kilipopata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Chelsea, na kufungua upya mbio za ubingwa wa Premier League.

MANCHESTER, ENGLAND: FURSA iliwekwa wazi mbele ya Manchester City, wangeitikiaje baada ya Arsenal kupoteza nyumbani Jumamosi dhidi ya Bournemouth?

Swali hilo lilijibiwa siku ya Jumapili, wakati kikosi cha Pep Guardiola kilipopata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Chelsea, na kufungua upya mbio za ubingwa wa Premier League.

Wakati Arsenal wakianza kuyumba, City wanaonekana kuimarika, na baada ya kupunguza tofauti hadi pointi sita nyuma ya vinara huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi, ishara zinaonekana kuwatisha vijana hao wa kaskazini mwa London.

Arsenal wanatarajiwa kuwa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa katikati ya wiki hii, lakini macho ya City sasa yako kwenye mechi ya Jumapili ijayo dhidi ya kikosi cha Mikel Arteta, wakitarajia kupunguza zaidi pengo la alama.

City wamekuwa katika kiwango bora katika michezo mitatu iliyopita, wakifunga mabao tisa dhidi ya Arsenal, Liverpool na Chelsea huku wakitoka uwanjani bila nyavu zao kutikiswa, wakitwaa Kombe la Carabao na kufika nusu fainali ya FA Cup katika kipindi hicho.

“Tumecheza vizuri mechi tatu, lakini timu bora England ni Arsenal na timu bora Ulaya ni Arsenal,” amesema Pep Guardiola.

“Namba zinaonyesha walivyokuwa thabiti. Tutajiandaa vizuri wiki hii.”


CITY NA ARSENAL HISTORIA INAJIRUDIA

“Arsenal mnatazama?” ilikuwa kauli iliyosikika kutoka kwa mashabiki wa City uwanjani.

Kama walikuwa wanatazama, basi ilikuwa kwa hofu, wakiona jinsi City wanavyoanza kushika kasi baada ya kuisambaratisha Chelsea katika mechi hiyo ya Premier ambayo kipindi cha kwanza kilikuwa 0-0, lakini kile cha pili kikawa cha maafa kwa vijana hao wa London.

Takwimu zinaonyesha mwezi Aprili ndio wenye mafanikio zaidi kwa Pep Guardiola na mbaya zaidi kwa Mikel Arteta, matokeo ya hivi karibuni yamethibitisha hilo.

City wamezoea kuwa wawindaji wa kileleni, hali ambayo Arsenal wanaijua vizuri. Msimu wa 2022-23, Arsenal waliongoza kwa siku 248 lakini wakashindwa kuchukua ubingwa.


CITY WANAZIDI KUIMARIKA

City hawajapoteza mechi tisa mfululizo za ligi na wamepoteza moja tu kati ya mechi 19 zilizopita, ishara kwamba wanaanza kufikia kilele kwa wakati sahihi.

Beki wa zamani wa Manchester United, Gary Neville amesema: “Manchester City wanahisi harufu ya ushindi. Wanajiandaa kwa pambano kubwa linalofuata.”


RATIBA YA MWISHO

Faida ndogo kwa Arsenal ni ratiba iliyobaki, wanakutana na timu zilizo chini ya msimamo. City wao watakutana na timu ngumu kama Everton, Brentford na Aston Villa.

Guardiola anasema: “Tukishinda dhidi yao (Arsenal), imekwisha. Hata sare inaweza kuwa hivyo.”

City pia wana mchezo mkononi dhidi ya Burnley, ambao wakishinda unaweza kuwapeleka kileleni.

Mwanzoni mwa msimu huu, Guardiola alibadilisha kikosi chake kwa kuondoa wachezaji wenye uzoefu kama Kevin De Bruyne, Ilkay Gundogan, Kyle Walker na Ederson.

Aliwaleta vijana kama Gianluigi Donnarumma na Rayan Cherki, pamoja na Marc Guehi na Antoine Semenyo.

Nahodha Bernardo Silva anaendelea kuiongoza timu hiyo, huku Rodri akirudi katika kiwango chake bora.

Ingawa Erling Haaland ndiye mfungaji bora akiwa na mabao 22, City wanaonyesha hawamtegemei sana yeye pekee.

Kutolewa kwa City kwenye Ligi ya Mabingwa kunawapa muda wa kujiandaa, tofauti na Arsenal ambao bado wanashiriki mashindano hayo.

Guardiola anasema: “Kuwa underdog ni kitu ninachokipenda. Hakuna aliyetuamini kwenye fainali ya Carabao Cup.”

Ameongeza kuwa, mafanikio yanahitaji si tu kushinda, bali pia kucheza vizuri na kuendelea kuboresha kiwango.

Ushindi mwingine dhidi ya Arsenal wikiendi hii utaonyesha wazi jinsi City walivyokua na kuimarisha nafasi yao ya kutwaa ubingwa.