Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majeruhi Arsenal wamvuruga Arteta

Muktasari:

  • Kocha Mikel Arteta anafahamu itakuwa ngumu kuvumilia majeraha wakati mwingine kwa kuwakosa wachezaji muhimu na hivyo timu inashindwa kutimiza malengo ya kubeba ubingwa.

LONDON, ENGLAND: ARSENAL imefanya usajili wa mastaa kibao kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi kwa kuhakikisha kwamba inakuwa na kikosi kipana kitakachopambana na masuala ya majeruhi.

Kocha Mikel Arteta anafahamu itakuwa ngumu kuvumilia majeraha wakati mwingine kwa kuwakosa wachezaji muhimu na hivyo timu inashindwa kutimiza malengo ya kubeba ubingwa.

Na sasa Arsenal imekuwa na imani kubwa kwenye upanda wa kikosi hicho kitaweza kukabiliana na ratiba ya mechi zijazowakabili. William Saliba aliumia mazoezini wakati akijiandaa kukabiliana na Chelsea na jambo hilo litamfanya kuwa nje ya uwanja kwa siku kadhaa.

Sambamba na hilo, Arsenal itamkosa beki wa kati mwingine, Gabriel, ambaye aliumia akiwa kwenye kikosi cha timu yake ya taifa ya Brazil. Kai Havertz yupo nje hajaanza kucheza na anaweza kurudi uwanjani kujifua muda si mrefu huku Leandro Trossard akisumbuliwa na maumivu ya kigimbi aliyopata mechi dhidi ya Bayern Munich.

Kwa sasa, Martin Odegaard, Viktor Gyokeres na Gabriel Jesus wamerejea uwanjani. Odegaard na Gyokeres walicheza dhidi ya Chelsea na walionekana kuwa moto uwanjani Stamford Bridge.

Jesus alifunga bao kwenye mechi ya kirafiki iliyochezwa bila mashabiki, hivyo muda wowote atarejea kwenye kikosi kuhakikisha Arsenal inatimiza malengo.

Hiyo ni habari njema kwa Arsenal hasa katika kipindi hiki ikielekea kwenye ratiba ngumu, ikikabiliana na Brentford, leo Jumatano, Aston Villa, Jumamosi na kisha itacheza kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe la Ligi.

Na hapo, Arteta atakuwa na muda wa kutosha kutoa nafasi kwa kila mchezaji katika kikosi ili timu ifanye vizuri katika michuano inayokabiliana nayo ikiwamo mpango wa ubingwa EPL