Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majanga! Majeruhi sita Arsenal wazua hofu

MAJANGA Pict

Muktasari:

  • Wikiendi iliyopita chama hilo la Mikel Arteta lilipoteza katika mechi ya fainali ya Kombe la Carabao kwa mabao 2-0 kutoka kwa Manchester City, huku ikiongeza idadi ya majeruhi.

LONDON, ENGLAND: BEKI wa Arsenal, Gabriel Magalhaes ameungana na nyota wengine watano wa kikosi hicho waliotemwa na timu zao za taifa kwa kuhofiwa kuwa majeruhi.

Wikiendi iliyopita chama hilo la Mikel Arteta lilipoteza katika mechi ya fainali ya Kombe la Carabao kwa mabao 2-0 kutoka kwa Manchester City, huku ikiongeza idadi ya majeruhi.

Kwa sasa ikiwa ligi zimesimama kupisha ratiba yaShirikisho la Soka Duniani (Fifa), wachezaji wamekuwa wakiitwa na timu zao za taifa kwa ajili ya mechi mbalimbali za kimataifa huku nyota sita wa Arsenal waliodhaniwa wataitwa wamepigwa chini.

Staa wa Brazil, Magalhaes ndiye wa mwisho katika listi hiyo na hayupo katika mazoezi ya timu yake ya taifa akiungana na William Saliba, Leandro Trossard, Jurrien Timber na Eberechi Eze na Martin Odegaard.

Nahodha wa Arsenal, Odegaard aliachwa nje ya kikosi cha Norway akiwa anaendelea kupona jeraha la goti, huku ukubwa wa majeraha ya nyota wengine ukiwa haujulikani kwa kila mmoja, ikielezwa kujitoa kwa Magalhaes, Saliba na Trossard ni kutokana na kuchukua tahadhari.

Magalhaes ambaye alijitoa katika kikosi cha Brazil cha Carlo Ancelotti kinachojiandaa na mechi za kirafiki dhidi ya Ufaransa na Croatia, anadai alipata maumivu ya goti la kulia katika fainali ya Carabao.

“Vipimo vya picha vimebaini Magalhaes hayupo tayari kucheza katika michezo hii wakati wa mapumziko ya kimataifa ya Fifa. Hakutakuwa na mchezaji mwingine wa kuitwa badala yake,” ilisema taarifa ya timu ya taifa ya Brazil.

Saliba ambaye alicheza pamoja na Gabriel katika safu ya ulinzi ya Arsenal, Jumapili, naye ameondoa jina lake kwenye kikosi cha Ufaransa, huku Maxence Lacroix wa Crystal Palace akiitwa kuchukua nafasi yake.

Maja 01

“Saliba hawezi kujiunga na kambi ya mazoezi ya timu ya taifa ya Ufaransa ambayo imeshaanza. Kiungo huyo wa kati wa Arsenal ana maumivu yanayojirudia kwenye kifundo cha mguu wa kushoto yanayohitaji matibabu na kipindi cha mapumziko cha angalau siku 10,” ilisema taarifa ya Shirikisho la Soka la Ufaransa.

Trossard ambaye alicheza dakika 82 za fainali ya Carabao, ameondoa jina lake kwenye kikosi cha Ubelgiji baada ya mazungumzo kati ya shirikisho la nchi hiyo na Arsenal na uamuzi huo ulitolewa baada ya tatizo la misuli lililojitokeza hivi karibuni.

Awali, ilitangazwa Eberechi Eze na Jurrien Timber walilazimika kuondolewa majina yao kutoka timu za England na Uholanzi mtawalia na wote wawili walikosa fainali ya Jumapili kutokana na majeraha.

Inatarajiwa Eze atafanyiwa vipimo wiki ijayo ili kubaini kiwango cha tatizo la misuli.

Ben White, hata hivyo, aliitwa kujiunga na England ikiwa ni mara ya kwanza tangu Kombe la Dunia 2022 Qatar.

White alichukua nafasi ya Jarell Quansah katika kikosi cha Thomas Tuchel kwa kambi ya mwisho kabla ya Kombe la Dunia msimu huu.

Beki huyo wa kulia aliondoka katika kambi ya Three Lions wakati wa hatua za makundi huko Qatar 2022 ikiwa ni siku moja baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Wales, huku FA ikieleza ni kwa “sababu binafsi”.

Inaripotiwa alikasirishwa na maoni ya kocha namba mbili wa England, Steve Holland na baadaye aliendelea kudai hatarudi katika kikosi hicho.

Kwa upande wa Odegaard amecheza mechi moja tu Arsenal tangu Februari 12, huku nahodha huyo wa Arsenal akipona jeraha la goti lililomuweka nje kwa mwezi mzima.

Wakati wa kutangaza kikosi cha Norway, wiki iliyopita, kocha Stale Solbakken alikiri kutokuwepo kwa Odegaard kama tahadhari huku akimwelezea kiungo huyo atakuwa katika kiwango cha juu kwa ajili ya Kombe la Dunia.

“Kitu muhimu zaidi ni awe amejipanga vizuri kadiri inavyowezekana na itakuwa upumbavu kusukuma kitu ambacho hatufikiri ni busara kwa sababu ataonekana. Tutaona kama ataonyesha (ubora), lakini si jambo tunalosukuma kwa lazima,” amesema Solbakken.

Baada ya kushindwa katika fainali ya Carabao, Arsenal watakabiliana na Southampton katika robo fainali za FA, Aprili 4, kabla ya kukabiliana na Sporting Lisbon siku tatu baadaye katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kisha watageukia Ligi Kuu England wanapokabiliana na Bournemouth Aprili 11.

Baada ya kukamilisha robo fainali za Ligi ya Mabingwa Aprili 15, mechi muhimu inayowezekana ni dhidi ya Man City katika Ligi Kuu, Aprili 19. Arsenal kwa sasa wako pointi tisa mbele ya Man City yenye mchezo mmoja mkononi.