Madrid yaanza kibingwa

Thursday February 25 2021
madrid pic

ATLANTA, ITALIA. MICHUANO ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya iliendelea jana katika hatua ya mtoano ya 16 bora na Real Madrid ikaanza vizuri kwa kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Atlanta ya Italia.
Madrid ilijipatia bao katika dakika ya 86 kupitia kwa Ferland Mendy aliyepokea pasi kutoka kwa Luka Modirc nje ya boksi  na kupiga mpira uliokwenda kugonga vyavu za upande wa kulia.
Ushindi huo umeiweka Madrid katika nafasi nzuri ya kuingia robo fainali kwa sababu mechi inayofuata itakua na faida ya kucheza kwenye uwanja wake wa nyumbani.

madrid pic 1


Manchester City nayo iliyokua ugenini ilifanikiwa kushinda ugenini dhidi ya Borussia Moenchengladbach iliposhinda mabao 2-0 katika dimba la Puskas Arena.

madrid pic 2


Mabao ya Manchester City yalifungwa na Bernardo Silva katika dakika ya 29 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Joao Cancelo, huku la pili likifungwa na Gabriel Jesus dakika ya 65 kwa pasi ya Bernardo Silva.
Mechi za  marudiano kati ya Madrid na Atlanta, Man City na Moenchengladbach zote zitapigwa Machi 17 mwaka huu.


Advertisement
Advertisement