Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Leroy Sane kutikisa vigogo Ulaya

Muktasari:

  • Sane, 28, alikuwa kwenye ubora mkubwa katika misimu yake minne huko Manchester City, mahali ambako alishinda mataji mawili ya Ligi Kuu England na Kombe la FA kabla ya kurudi kwao Ujerumani kujiunga na Bayern mwaka 2020.

MUNICH, UJERUMANI: LISEMWALO ni kwamba Manchester United na Chelsea zinatajwa kupigana vikumbo chinichini kwenye vita ya kusaka saini ya staa wa Bayern Munich, Leroy Sane.

Sane, 28, alikuwa kwenye ubora mkubwa katika misimu yake minne huko Manchester City, mahali ambako alishinda mataji mawili ya Ligi Kuu England na Kombe la FA kabla ya kurudi kwao Ujerumani kujiunga na Bayern mwaka 2020.

Hata hivyo, mkataba wa winga huyo utakwisha Juni mwakani na hakuonekani kuwapo na mpango wa kusaini dili jipya huko Allianz Arena.

Na sasa kinachoripotiwa ni kwamba kuzorota kwa mazungumzo ya dili jipya baina ya pande hizo mbili kumechochea klabu nyingine kufukuzia saini ya Sane.

Kati ya timu hizo ni Man United, Chelsea sambamba na Tottenham huku ikielezwa mitego yote imewekwa kwa ajili ya dirisha la Januari.

Lakini, miamba hiyo mitatu ya Ligi Kuu England, itakabiliwa na vita kali kutoka kwa Barcelona, ambao pia wameonyesha dhamira ya kumnasa Sane.

Barca inahitaji winga mwenye kiwango cha juu baada ya kumpoteza mkali wao, Lamine Yamal kutokana na kuwa majeruhi. Barcelona pia inahitaji saini ya mkali wa Napoli, Khvicha Kvaratskhelia, wa AC Milan, Rafael Leao na wa Athletic Bilbao, Nico Williams.

Hali mbaya ya kiuchumi inafanya Barca kutokuwa na nguvu kwenye kushindania saini za wachezaji hao na hivyo kuna uwezekano ikakwama kwenye mpango wake. Bayern Munich yenyewe haina shida kwenye kuachana na Sane kwani kwenye kikosi chao kuna mawinga wa kutosha akiwamo Jamal Musiala, Serge Gnabry, Michael Olise na Kingsley Coman. Sane amefunga mabao manne na asisti moja kwenye mechi 19 alizocheza msimu huu.