Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lampard anapata kile anachostahili

LAMPAARD Pict

Muktasari:

  • Heshima hiyo haijatokana na kushinda mataji lukuki ya Ligi Kuu England kama ilivyokuwa kwa Sir Alex Ferguson na makocha wengi, bali imesababishwa na uwezo wake mkubwa kuziokoa timu zisishuke daraja.

LONDON, ENGLAND: KWENYE maktaba ya majina ya makocha ambao hawakuwa na mafanikio makubwa katika Ligi Kuu England lakini wana heshima hadi sasa, mmoja ni Sam Alladyce ‘Big Sam’.

Heshima hiyo haijatokana na kushinda mataji lukuki ya Ligi Kuu England kama ilivyokuwa kwa Sir Alex Ferguson na makocha wengi, bali imesababishwa na uwezo wake mkubwa kuziokoa timu zisishuke daraja.

Mara zote ambazo timu ziliona zinaenda kushuka daraja, Big Sam alikuwa akiitwa na kupewa kazi na baada ya hapo ilikuwa lazima aziondoe katika janga hilo.

Ukienda katika kumbukumbu za Blackburn Rovers, Sunderland na Crystal Palace zote ziliwahi kusaidiwa na Big sam kutoshuka daraja baada ya kuanza msimu vibaya.

Ni mara moja tu, aliwahi kushindwa kufanya hivyo msimu wa 2022-23 alipopewa kazi hiyo na Leeds United na tangu hapo hakuwahi kuonekana tena akifundisha timu yoyote.

Maisha ya Big Sam yanaturudisha kwa rafiki yetu Lampard. Hakuwahi kuwa na bahati hata kidogo alipojaribu kuwa kocha wa timu za Ligi Kuu England.

Baada ya kuwa na rekodi mbaya Chelsea, ilisemwa pengine ni kwa sababu ya ukubwa wa timu, lakini hata alipopewa mikoba ya kuifundisha Everton, mambo yaliendelea kuwa vilevile. Inawezekana ikawa ni bahati au upepo, lakini hakuna kilichowahi kufanikiwa chini yake alipojaribu EPL.

Hata hivyo, mambo huwa tofauti pale anapokuwa Championship, akiwa na Derby County alifanikiwa kwa kiasi chake hadi akaipeleka timu hiyo katika mechi za mtoano kuwania kupanda Ligi Kuu baada ya kumaliza katika nafasi sita za juu.

Licha ya kutofanikiwa kuipandisha, Chelsea iliona alichofanya na ikamwajiri lakini bado mambo yalikuwa tofauti na hata alipoajiriwa kwa mara ya pili kama kocha wa muda bado hakuna mafanikio yoyote aliyoipa timu hiyo.

Baada ya kuzunguka sana kwa sasa amerejea tena Championshi akiwa na Converty City.

Msimamo unaonyesha timu hiyo inaongoza kileleni kwa tofauti ya alama 10 dhidi ya Stoke City na Middlesbrough zinazoshika nafasi ya pili na tatu.

Hayo ni mafanikio makubwa kwa timu ambayo msimu uliopita ilimaliza nafasi ya tano katika msimamo na ikaenda kutolewa katika mechi ya kwanza tu ya mtoano wa kugombania kupanda daraja.

Lampard ni kama amerudi nyumbani, Championship inaonekana kumkubali kama zilivyokuwa zinamkubali timu zinazokaribia kushuka daraja Sam Allardyce.

Katika mechi 20 za mwisho za michuano yote, Lampard ambaye alijiunga na timu hii Novemba mwaka jana, ameiwezesha kushinda 12, sare tano na kufungwa mbili na hadi sasa  imecheza jumla ya mechi nne mfululizo na kushinda zote na ingekuwa na jumla ya mechi 12 ikiwa isingepoteza mbele ya Wrexham.