Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kumbe Haaland anachota maujuzi kwa Solskjaer

Muktasari:

  • Straika huyo wa kimataifa wa Norway tayari ameshafunga mabao 25 kwenye kikosi hicho cha kocha Pep Guardiola msimu huu na kuisaidia timu yake ya taifa kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026.

MANCHESTER, ENGLAND: STRAIKA wa mabao, Erling Haaland amesema amekuwa akichota ujuzi kutoka kwa Ole Gunnar Solskjaer ili kuhakikisha Manchester City imefikia malengo yao makubwa ya kunyakua taji la Ligi Kuu England.

Straika huyo wa kimataifa wa Norway tayari ameshafunga mabao 25 kwenye kikosi hicho cha kocha Pep Guardiola msimu huu na kuisaidia timu yake ya taifa kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026.

Haaland, 25, alifunga mara mbili dhidi ya West Ham, Jumamosi iliyopita. Lakini, straika huyo bado anatafuta njia ya kuwa bora zaidi ndani ya uwanja kwenye masuala ya kufunga mabao hasa katika kuelekea mechi ijayo dhidi ya Nottingham Forest itakayopigwa Jumamosi.

Staa Haaland alishea posti yake ya Instagram akionyesha picha aliyopiga na gwiji wa Manchester United, Solskjaer. Kwenye picha hiyo, Haaland aliandika maneno haya, “maarifa”, akiwa na maana amekwenda kuchota ujuzi kwa kocha wake huyo wa zamani. Na mchezaji Jack Grealish, ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo Everton, alikomenti: “Ole Gunnar Knowledge.”

Solskjaer amekuwa na ufahamu wa namna ya kufunga mabao dhidi ya Nottingham Forest. Kwenye vitabu vya rekodi vinaonyesha Solskjaer alifunga mabao manne katika ushindi wa 8-1 ilioupata Man United dhidi ya Forest enzi hizo alipokuwa mchezaji huku kwenye mechi hiyo alitokea benchini na kuingia katika dakika 72.

Solskjaer, 52, aliwahi kumnoa Haaland walipokuwa pamoja kwenye kikosi cha Molde ya Norway. Na tangu wakati huo wamekuwa wakiwasiliana licha ya kwamba Haaland kwa sasa anakipiga kwenye kikosi cha mahasimu wa Man United, Man City.