Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kroos afurahia ushindi wa El Clasico, ampongeza Xabi Alonso

Kroos Pict

Muktasari:

  • Wenyeji Real Madrid walichomoza na ushindi wa 2-1, mabao yalifungwa na Kylian Mbappe na Jude Bellingham, huku bao la Barcelona likifungwa na Fermin Lopez. Yote kipindi cha kwanza.

Aliyekuwa kiungo wa Real Madrid, Toni Kroos, amesema timu hiyo ilikuwa na nafasi ya kufunga mabao mengi kwenye mechi ya El Clásico, iliyopigwa juzi Jumapili, Oktoba 26, 2025 kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu, mjini Madrid.

Wenyeji Real Madrid walichomoza na ushindi wa 2-1, mabao yalifungwa na Kylian Mbappe na Jude Bellingham, huku bao la Barcelona likifungwa na Fermin Lopez. Yote kipindi cha kwanza.

Kroos ambaye aliitumikia Real Madrid kuanzia mwaka 2014 hadi 2024, amesema Los Blancos ilistahili ushindi dhidi ya Barcelona, huku akimsifu kocha Xabi Alonso kwa mbinu nzuri alizotumia kwenye mechi hiyo.

Akizungumza kupitia podcast yake Einfach mal Luppen, Kroos amesema Real Madrid ilitumia vyema upungufu wa mbinu za Barcelona, na kwamba ushindi huo ulikuwa wa haki. 

Kro 01

“El Clásico? Nimefurahi sana kwamba Real Madrid imeshinda. Ni ushindi waliostahili kabisa. Walitumia vizuri mbinu za kuishinda Barcelona. Matokeo yangekuwa makubwa zaidi kipindi cha kwanza. Real Madrid iliingia kwenye mechi hii kwa akili na mbinu bora.”

Kuhusu hisia za Vinícius Jr baada ya kutolewa uwanjani, Kroos amepingana na wanaomkosoa mchezaji huyo, akisema hawajui hisia za kucheza mbele ya mashabiki 80,000. Kiungo huyo wa zamani wa Madrid amemtetea Mbrazil huyo, akisema hata yeye hakuwahi kufurahia kutolewa kwenye mechi.

“Ukicheza mechi kubwa kama hii, hasa ukiwa katika kiwango kizuri, ni kawaida kutofurahia kutolewa. Hata mimi sikuwa napenda kubadilishwa. Ingawa kwa uaminifu, sikuwahi kuondoka moja kwa moja kuelekea vyumba vya kubadilishia nguo.

Kro 02

“Watu wanaweza kuhukumu kutoka nje, lakini napenda kusisitiza jambo hili, hakuna mtu anayeweza kuelewa hisia hizo isipokuwa yule aliye uwanjani, katika El Clásico, mbele ya watu 80,000, timu ikiwa inaongoza 2-1, unataka kufanya kila kitu ila tu usitolewe. Hizo hisia ni ngumu kuelezeka, na wengi wanaokosoa hawajawahi kupitia hali kama hiyo,” amesema.

Katika mechi hiyo, Kylian Mbappé na Jude Bellingham walifunga mabao ya Real Madrid kipindi cha kwanza, huku Fermín López akipachika bao pekee la Barcelona. Mbappé alipata nafasi ya kufunga tena kipindi cha pili kupitia penalti, lakini shuti lake liliokolewa na Wojciech Szczęsny.