Sikia hii ya Vini Jr kwenye Ballon d’Or
Muktasari:
- Staa huyo wa Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil amekuwa na msimu bora kabisa kwa 2023/24 na alifunga mabao 24 na kuasisti mara 11 wakati chama lake la Los Blancos kilienda kushinda ubingwa wa La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
MADRID, HISPANIA: NOMA sana. Linalosemwa ni Vinicius Junior tayari anafahamu atashinda tuzo ya Ballon d’Or ya mwaka huu, ripoti za kutoka Hispania zinafichua.
Staa huyo wa Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil amekuwa na msimu bora kabisa kwa 2023/24 na alifunga mabao 24 na kuasisti mara 11 wakati chama lake la Los Blancos kilienda kushinda ubingwa wa La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kiungo wa Manchester City, Rodri na mchezaji mwenzake Vinicius huko kwenye kikosi cha Real Madrid, Jude Bellingham wanatajwa pia kuwa na nafasi kubwa ya kushinda tuzo hiyo ya Ballon d’Or.
Hata hivyo, kwa mujibu wa Marca, Vinicius ameshapewa taarifa atashinda tuzo hiyo katika sherehe zitakazofanyika Oktoba 28.
Kama hilo litatimia, basi Mbrazili huyo atakuwa mchezaji wa nne tofauti wa Real Madrid kushinda tuzo hiyo ndani ya miaka saba ya karibuni.
Ataungana na kundi la magwiji Cristiano Ronaldo, Luka Modric na Karim Benzema.
Lionel Messi ni mchezaji pekee asiyekuwa wa Real Madrid katika kipindi cha miaka 15 ya mwisho ameshinda tuzo hiyo ya Ballon d’Or - akibeba mara nane kati ya mwaka 2009 na 2023.
Akijumuishwa na kiungo Toni Kroos, aliyestaafu soka baada ya kuondoka Real Madrid mwishoni mwa msimu uliopita, Vinicius ni mmoja kati ya wachezaji sita wa Los Blancos waliopo kwenye orodha hiyo ya wakali 30 wanaoshindania tuzo hiyo ya Ballon d’Or kwa upande wa wanaume.
Bellingham, Kylian Mbappe, Antonio Rudiger na Fede Valverde nao ametajwa kwenye orodha hiyo baada ya kuisaidia timu yao ya Real Madrid kubeba taji la 15 la Ulaya msimu uliopita. Wabrazili waliowahi kushinda tuzo hiyo ya Ballon d’Or ni Ricardo Kaka, Ronaldo Nazario, Ronaldinho na Rivaldo.